Spelling suggestions: "subject:"afrika"" "subject:"suidafrika""
1 |
Utata katika ubainishaji wa fasihi ya watoto kwa kurejelea kitabu cha Mgomba ChangaraweniMalugu, Alfred 12 September 2022 (has links)
Fasihi ya watoto hujipambanua kwa kupitia sifa mintarafu dhidi ya fasihi ya watu wazima. Miongoni mwa sifa hizi, ni zile zilizobainishwa na wataalamu kama Mulokozi (2017), Schneider (2016), Bakize (2014, 2015), Lynch-Brown na wenzake (2014), Stakic (2014), Matundura na wenzake (2013), na Wamitila (2010); tukiwataja kwa uchache tu. Kwa jumla, wataalamu hawa wanabainisha sifa mahsusi zinazofungamana na kazi za fasihi zinazoingia katika kumbo la fasihi ya Watoto. Kitabu cha Mgomba Changaraweni (2005) kilichoandikwa na Ken Walibora kinatambulika kuwa ni miongoni mwa vitabu vya fasihi ya watoto nchini Kenya. Licha ya kitabu hicho kutambuliwa kama fasihi ya watoto, tunaporejelea sifa za fasihi ya watoto kulingana na wataalamu mbalimbali tuliyowataja hapo awali, tunaona kuwa kitabu hiki kina sifa nyingi za fasihi ya watu wazima kuliko fasihi ya watoto. Kwa hivyo basi, tunaonelea kuwa, kitabu hiki kinafaa zaidi kuingia katika kumbo la fasihi ya watu wazima kuliko kuingizwa katika kumbo la fasihi ya watoto. Katika makala haya, tutahakiki kitabu hiki ili kuangalia ni kwa vipi kinaibua utata katika kukubaliana kuwa kinastahili kuwekwa katika kumbo la fasihi ya watoto.
|
Page generated in 0.0437 seconds