• Refine Query
  • Source
  • Publication year
  • to
  • Language
  • 1
  • Tagged with
  • 1
  • 1
  • 1
  • 1
  • 1
  • 1
  • 1
  • 1
  • 1
  • 1
  • 1
  • 1
  • 1
  • 1
  • 1
  • About
  • The Global ETD Search service is a free service for researchers to find electronic theses and dissertations. This service is provided by the Networked Digital Library of Theses and Dissertations.
    Our metadata is collected from universities around the world. If you manage a university/consortium/country archive and want to be added, details can be found on the NDLTD website.
1

Maenezi ya Lugha ya Kiswahili Nchini Sudan Kusini: Mafanikio na Changamoto

Habwe, John Hamu 30 May 2022 (has links)
Utafiti huu unachunguza maenezi ya lugha ya Kiswahili katika taifa la Sudan Kusini kwa kuangazia njia zilizotumika kuisambaza hii lugha ya Kiswahili nchini humo. Unachunguza pia changamoto za lugha ya Kiswahili nchini Sudan Kusini na mustakabali wake. Data ya utafiti huu imekusanywa nyanjani kupitia kifaa cha mahojiano ambapo tuliwahoji wenyeji wa Sudan Kusini na wafanyakazi wa mashirika mbalimbali nchini Sudan Kusini. Utafiti huu umebaini kuwa Kiswahili kimeingia Sudan Kusini kwa msaada wa nyenzo mbalimbali kama vile vita, biashara, elimu, maingiliano ya mipakani, dini na ndoa. Utafiti huu pia unajadili baadhi ya vizuizi vinavyoweza kutatiza ukuaji na ueneaji wa Kiswahili katika taifa la Sudan Kusini kama vile tishio kubwa la ushindani na upinzani wa makundi ya lugha za Sudan Kusini na lugha ya Kiarabu ambayo ndiyo lugha ya maenezi mapana, na hali kadhalika lugha ya Kiingereza ambayo ni moja katika lugha zinazoenziwa katika taifa la Sudan Kusini hasa kwa kuwa lugha ya kimataifa. Imebainika pia kuwa sababu kubwa za kujifundisha Kiswahili kwa wenyeji wengi wa Sudan Kusini kumechangiwa na haja ya kutaka kujitambulisha na kujinasibisha na makundi mbalimbali ya Afrika Mashariki. Utafiti huu unahoji pia kuwa mustakabali wa lugha ya Kiswahili utategemea sera ya lugha nchini Sudan Kusini na utekelezaji wa matakwa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya kufanya Kiswahili kuwa lugha ya maenezi mapana katika eneo la Afrika Mashariki nakopatikana nchi ya Sudan Kusini. / This paper examines the spread of Swahili to South Sudan. It explores the challenges of the language in South Sudan and its potential future status and use. Data from this study were collected through interviews with South Sudanese residents and employees of various organizations. The study reveals that Swahili has gained ground in South Sudan due to war, trade, education, cross-border interaction, religion and marriage practices. This study also discusses some of the impeding barriers to the growth and spread of the language, e.g., with reference to the status and use Arabic and English. It is also observed that among the main reasons for learning Swahili for many South Sudanese people is the need to identify with other East Africans. The study also argues that the future of the language will depend on the language policies in South Sudan and the implementation of the East African Community's aspirations to make Swahili a widespread language beyond its core regions.

Page generated in 0.0436 seconds