Return to search

Ujuzi wa watoto/vijana katika simulizi za maisha

Kutoka elimu ya lugha tunajua kwamba kila mtu aliyenena ana ujuzi maalum - kama John Lyons alivyoeleza katika kitabu chake Language and Linguistics (1981), katika sura kuhusu lugha na utamaduni wa wasemaji. Lyons anatueleza kwamba kila mtu hushika ujuzi huo kwa njia ya kufunzwa lugha na huutumia ujuzi, huuongeza na huubadilisha kwa muda wa maisha yake yote; ni jinsi yake ya kujua mambo ya ulimwengu. Katika maelezo yafuatayo napenda kuonyesha ujuzi uliomo katika habari nilizopewa na kijana, jina lake ni Timothy Lawrence ambaye alikuwa na umri wa kumi na tatu siku zile. Ujuzi wake ni juu ya maisha yake ya kipokomo na pia ni ujuzi wa kumweleza mgeni mambo hayo - yaani ujuzi au uwezo wa kuzisimulia habari hizo. Habari zake zinatuonyesha vizuri simulizi ya maisha ya binafsi (au autobiographical narrative) ni nini, yenye ujuzi gani na jinsi gani ya kutazama maisha kwa macho ya mwenyeji kijana.

Identiferoai:union.ndltd.org:DRESDEN/oai:qucosa:de:qucosa:11790
Date14 December 2012
CreatorsSchulz-Burgdorf, Ulrich
ContributorsUniversität zu Köln
Source SetsHochschulschriftenserver (HSSS) der SLUB Dresden
LanguageSwahili
Detected LanguageUnknown
Typedoc-type:article, info:eu-repo/semantics/article, doc-type:Text
SourceSwahili Forum; 4(1997), S. 95-105
Rightsinfo:eu-repo/semantics/openAccess
Relationurn:nbn:de:bsz:15-qucosa-97269, qucosa:11675

Page generated in 0.0054 seconds