Makala hii inachanganua wahusika na dhana kuu zinazosawiriwa katika riwaya ya Kiza Katika Nuru (1988) ya Said Ahmed Mohamed kwa kuzingatia mihimili ya mojawapo ya mikabala ya Umarxi Mpya, mkabala wa mwanafalsafa na mwananadharia kutoka Marekani ya Kilatini, Paulo Freire. Kiini cha mkabala huu wa umarxi-mpya ni kukosoa na kutupilia mbali mitazamo kuhusu elimu inayomnyima mwanafunzi fursa ya kujifunza kutokana na mazingira yake. Uchambuzi huu unabainisha jinsi Umarxi Mpya wa Kifreire unavyofaa kwa kuchambua riwaya ya Kiza Katika Nuru, na riwaya nyingine za Kiswahili zinazofanana nayo. / This article analyses characters and main concepts in Said Ahmed Mohamed’s novel Kiza katika Nuru (Darkness in Light) through applying tenets of one of the Neo-Marxist theories, namely the Freirean one. Paul Freire’s Neo-Marxist theory is primarily associated with the Latin American environment and centres around the debunking of the banking concept education as a modus operand of revolution. This analysis demonstrates how Freirean Neo-Marxism is relevant and appropriate to the understanding and interpretation of Kiza Katika Nuru and other Kiswahili novels that are similar to it.
Identifer | oai:union.ndltd.org:DRESDEN/oai:qucosa:de:qucosa:79295 |
Date | 30 May 2022 |
Creators | Wafula, Richard Makhanu, Mue, Elizabeth Kasau |
Contributors | Universität Leipzig |
Source Sets | Hochschulschriftenserver (HSSS) der SLUB Dresden |
Language | Swahili |
Detected Language | Unknown |
Type | info:eu-repo/semantics/publishedVersion, doc-type:article, info:eu-repo/semantics/article, doc-type:Text |
Rights | info:eu-repo/semantics/openAccess |
Relation | 1614-2373, urn:nbn:de:bsz:15-qucosa2-792924, qucosa:79292 |
Page generated in 0.0023 seconds