Vitendawili vya Kiswahili, kama vitendawili katika lugha nyingine za Kibantu, na kwa hakika katika lugha nyingine za Kiafrika, ni mafumbo ambayo hutolewa kama kauli au swali linalotaka jibu (Gowlett 1979; Harries 1971, 1976; Okpewho 1992). Vitendawili katika Kiswahili ni sehemu muhimu sana ya michezo ya watoto. Katika jamii ambazo bado zinaishi maisha ya jadi, watoto hukaa pamoja jioni pengine wakiwa na dada zao, kaka zao, na binamu zao wakasimuliana hadithi na kutegana vitendawili. Makala hii inachunguza muundo wa visabiki vya vitendawili vya Kiswahili na kutokana na mchangamano wa muundo tunapendekeza kwamba vitendawili ni njia kuu ya kufundisha watoto ufasaha wa lugha. Ukichunguza usambamba katika vitendawili utaona changamoto kubwa hutolewa kwa mtegaji na wasikilizaji wake kutokana na usambamba ulioko katika sintaksia, fonolojia, kadhalika sitiari. Kama Scheub (2002:124) asemavyo: «Vitendawili ni modeli kwa ajili sanaa za lugha».
Identifer | oai:union.ndltd.org:DRESDEN/oai:qucosa:de:qucosa:11737 |
Date | 03 December 2012 |
Creators | Ngonyani, Deo |
Contributors | Michigan State University, Universität Mainz |
Source Sets | Hochschulschriftenserver (HSSS) der SLUB Dresden |
Language | Swahili |
Detected Language | Unknown |
Type | doc-type:article, info:eu-repo/semantics/article, doc-type:Text |
Source | Swahili Forum; 12(2005), S. 121-132 |
Rights | info:eu-repo/semantics/openAccess |
Relation | urn:nbn:de:bsz:15-qucosa-94062, qucosa:11593 |
Page generated in 0.0474 seconds