Return to search

Traditional Dances and Bongo Fleva: a Study of Youth Participation in Ngoma Groups in Tanzania

Kasi ya vijana katika kukuza muziki wa kizazi kipya katika kipindi cha utandawazi haiendani na kasi ya ukuzaji wa ngoma za asili. Mpaka sasa haujafanyika utafiti wa kina kuhusu kuzuka kwa tabia hii. Makala haya yanatumia mahojiano na vikundi vya ngoma vitatu halikadhalika wanamuziki wa kizazi kipya kuweka bayana chanzo cha tatizo. Aidha, makala haya yanatumia nadharia ya utendaji kama darubini kuchunguza matatizo ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni yanayowakumba vijana na namna yanavyochochea mfumuko wa tabia hii mpya. Utafiti huu umegundua kwamba uhaba wa mianya ya kiuchumi na kisiasa kwa vijana, nafasi ya ngoma za asili katika jamii ya sasa, mahusiano hasi kati ya vijana na wazee katika kuuendeleza utamaduni pamoja na vijana kutaka maendeleo ya haraka kuwa ndio chimbuko la tatizo.

Identiferoai:union.ndltd.org:DRESDEN/oai:qucosa.de:bsz:15-qucosa-137461
Date27 March 2014
CreatorsSanga, Daines
ContributorsUniversität Bayreuth, Institut für Afrikastudien, Universität Leipzig, Institut für Afrikanistik
PublisherUniversitätsbibliothek Leipzig
Source SetsHochschulschriftenserver (HSSS) der SLUB Dresden
LanguageEnglish
Detected LanguageUnknown
Typedoc-type:article
Formatapplication/pdf
SourceSwahili Forum 20 (2013), S. 67-84

Page generated in 0.0025 seconds