Return to search

W. E. Taylor (1856-1927):

Bwana Tela (1856-1927) alikuja Afrika ya mashriki kutoka Ulaya katika mwaka 1297 wa hijti (mwaka 1880 wa miladi), akakaa kwa muda wa myaka khamustaashara takriban. Ingawa alikuja kutangaza dini ya kiNasara, kazi aliyofanya zaidi Mambasa ilikuwa ni ya mambo ya utaalamu wa lugha ya kiSawahili, na mashairi yake, na utamaduni wa waSawahili. Alipata bahati ya kuwa na marafiki wataalamu wa kiMvita, khaswa Mwalimu Sikujuwa al-Batawi, na Bwana Hemedi al-Mambasi. Nyimbo zake za kiMisheni alizotunga kwa kiSawahili hazikutiwa maanani, lakini mahadhi aliokuwa akiimbiya yalibakiya kwa myaka mingi kwa jina la `mahildhi ya Tela´. Bwana Tela alisaidiana na Mwalimu Sikujuwa kuhifadhi t´ungo za washairi wengi wa kale zisipotee, khaswa t´ungo za Bwana Muyaka. Kadhalika alikusanya mithali ya kiSawahili, zaidi ya sita-mia. Karatasi zake alizoandika mambo ya kiSawahili, nyingi sasa ziko maktaba ya SOAS, London, na ni muhimu katika kutusaidiya kufahamu kiSawahili cha kiSawahili. Si makosa kusema kuwa Bwana Tela ndiye mtaalamu mkubwa wa kiSawahili katika wataalamu wote wa kiNgereza.

Identiferoai:union.ndltd.org:DRESDEN/oai:qucosa.de:bsz:15-qucosa-97777
Date30 November 2012
CreatorsFrankl, J.L.P.
ContributorsUniversität zu Köln, Institut für Afrikanistik
PublisherUniversitätsbibliothek Leipzig
Source SetsHochschulschriftenserver (HSSS) der SLUB Dresden
LanguageEnglish
Detected LanguageUnknown
Typedoc-type:article
Formatapplication/pdf
SourceSwahili Forum; 6(1999), S. 161-174

Page generated in 0.0015 seconds