Chachage Seithy L. Chachage amepata kuandika riwaya nyingine tatu: Sudi ya Yohana (1980), Kivuli (1984) na Almasi za Bandia (1990). Riwaya yake ya nne Makuadi wa Soko Huria (2002) ni ya kihistoria na yenye upekee wa maudhui, muundo na mtindo. Vipengele hivi vinadhihirisha ukomavu na upeo wa juu wa mwandishi ilimradi kwenda sambamba na changamoto ya utandawazi ya karne ya ishirini na moja ya milenia ya tatu. Mwandishi amekitabaruku kitabu hiki kwa kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (1922-1999).
Identifer | oai:union.ndltd.org:DRESDEN/oai:qucosa.de:bsz:15-qucosa-98242 |
Date | 30 November 2012 |
Creators | Mbonde, John P. |
Contributors | Universität Mainz, Insitut für Ethnologie und Afrikastudien |
Publisher | Universitätsbibliothek Leipzig |
Source Sets | Hochschulschriftenserver (HSSS) der SLUB Dresden |
Language | Swahili (individual language) |
Detected Language | Unknown |
Type | doc-type:article |
Format | application/pdf |
Source | Swahili Forum; 11(2004), S. 211-226 |
Page generated in 0.0021 seconds