Return to search

Kukitandawazisha Kiswahili kupitia simu za kiganjani: tafakari kuhusu isimujamii

Mojawapo ya matokeo ya utandawazi ni kuwapo kwa simu za kiganjani na matumizi yake. Siku hizi nchini Tanzania mawasiliano ya simu yamekuwako kwa wingi kuliko ilivyokuwa tangu wakati wa uhuru hadi katikati ya miaka ya tisini. Lugha ya Kiswahili inayotumika katika simu hizi ni ya kiutandawazi na pengine si rahisi kuiona nje ya wigo huu wa kiutandawazi ambao pia unajumuisha mawasiliano kwa barua pepe, na maongezi katika tovuti. Suala kubwa tunalolijadili katika makala hii ni changamoto zinazoletwa na lugha hii katika Isimujamii, hasa kuchanganya msimbo (lugha) na kubadili misimbo (lugha) (code mixing and code switching). Kwahiyo mwelekeo wa makala hii ni utafiti wa matumizi ya lugha hii tandawazi kwa kuangalia simu za viganjani na athari yake katika nadharia za isimujamii. Madhumuni yetu ni kuangalia matumizi ya lugha ya Kiswahili katika simu za viganjani.

Identiferoai:union.ndltd.org:DRESDEN/oai:qucosa.de:bsz:15-qucosa-98395
Date03 December 2012
CreatorsMutembei, Aldin
ContributorsChuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, Universität Mainz, Insitut für Ethnologie und Afrikastudien
PublisherUniversitätsbibliothek Leipzig
Source SetsHochschulschriftenserver (HSSS) der SLUB Dresden
LanguageSwahili (individual language)
Detected LanguageUnknown
Typedoc-type:article
Formatapplication/pdf
SourceSwahili Forum; 18(2011), S. 198-210

Page generated in 0.0024 seconds