Return to search

Matumizi Mema ya Viakifishi katika Uimarishaji wa Mawasiliano katika Lugha ya Kiswahili: Mfano wa Riwaya ya Mkamandume

Lugha ni nyenzo muhimu katika mchakato wa mawasiliano, hali inayoifanya nyenzo hii kuweza kuchanganuliwa kwa njia mbalimbali. Katika jitihada za kuichunguza na kuichanganua lugha, imebainika kwamba kuna uhusiano wa ufaano kati ya miundo ya lugha na dhima yake. Huu ndio uhusiano ambao hutumiwa na wasanii kifasihi kuunganisha mifumo ya lugha inayotumika katika matini na kuafikia ruwaza zao. Hali hii inatokana na uwezo wa kufulikana kwa lugha kama chombo cha mawasiliano ambao pia unaipa lugha uwezo wa kusukwa tofauti kwa mujibu wa dhima tofauti na hivyo basi kuendeleza grafolojia. Grafolojia ni mojawapo ya viwango vya uchanganuzi wa kiisimu kimtindo. Hata hivyo, umuhimu na nafasi ya grafolojia kama kiwango cha uchanganuzi wa matini hudhihirika katika umitindo na mbinu mseto. Kwa hali hiyo, watalaam wengi wakiwemo Halliday, McIntosh na Strevens (1964) wamefanya utafiti kuhusu jinsi mchepuko wa kigrafolojia unavyoathiri ufasiri kimaana na kuzalisha athari zingine za kiujumi katika matini. Miongoni mwa vipengele vya kigrafolojia ambavyo wamevitaja kwamba vinaibua athari tofauti katika matini ni viakifishi. Ingawa uandishi wowote, uwe wa jadi au wa leo unahitaji kuzingatia matumizi mema ya viakifishi, hivi leo kumeshuhudiwa ukiukaji wa matumizi ya vipengele hivi katika shughuli za kijamii. Ni kwa ajili hii ndiposa makala haya yameandaliwa yakilenga kuchanganua aina mbalimbali za viakifishi, herufi kubwa na mchango wa alama hizi katika uimarishaji wa mawasiliano katika lugha ya Kiswahili. Aidha makala haya yametayarishwa kwa kuchanganua yaliyomo katika riwaya ya kisasa ya Mkamandume (2013) huku nadharia ya Sarufi Amilifu Mfumo (SAM) iliyoasisiwa na Halliday ikiongoza utafiti huu. / Language is an important tool in communication. In an effort to explore and analyze language, it has been observed that there is a correlation between language structures and stylistic choices. Also used by literary artists who integrate these principles of in their text, graphology is one of the standards of linguistic analysis in style. However, its importance and place as a standard for textual analysis is manifested in a variety of styles and techniques. In this context, many scholars including Halliday, McIntosh and Stevens (1964) have done research on how grammatical “abnormalities' affect interpretation and produce other metaphorical effects in texts. This article aims at analyzing the different types of signs and conventions, abbreviations, practices of capitalization and the contribution of these symbols in strengthening communication in Swahili. In addition, this article uses the content of the novel Mkamandume (2013) and refers back to the basics of 'Sarufi Amilifu Mfumo' (SAM) developed by Halliday.

Identiferoai:union.ndltd.org:DRESDEN/oai:qucosa:de:qucosa:79296
Date30 May 2022
CreatorsMusotsi, Eliud Teyie, Miruka, Frida Akinyi, Okal, Bernard Odoyo
ContributorsUniversität Leipzig
Source SetsHochschulschriftenserver (HSSS) der SLUB Dresden
LanguageSwahili
Detected LanguageUnknown
Typeinfo:eu-repo/semantics/publishedVersion, doc-type:article, info:eu-repo/semantics/article, doc-type:Text
Rightsinfo:eu-repo/semantics/openAccess
Relation1614-2373, urn:nbn:de:bsz:15-qucosa2-792924, qucosa:79292

Page generated in 0.0017 seconds