Return to search

Sitiari katika Kichomi – Uchambuzi wa Mojawapo ya Mbinu za Kifasihi za Euphrase Kezilahabi*

Makala hii inachambua sitiari katika Kichomi, diwani ya kwanza ya marehemu Euphrase Kezilahabi. Mashairi yaliyochunguzwa yanahusika na dhamira tatu za kijumla: maana ya maisha, udhalimu wa kikoloni, na hali ya sasa ya Afrika. Mashairi yanayochambuliwa ni: “Nimechoka”, “Mwamba Ziwani”, “Fungueni Mlango”, na “Kisu Mkononi” (dhamira ya “maana ya maisha”); “Hadithi ya Mzee” (dhamira ya “udhalimu wa kikoloni”); “Afrika na Watu Wake”, “Kumbe”, na “Namagondo” (hali ya sasa ya Afrika). Mashairi haya yako kwenye muundo usiofuata urari wa vina na mizani. Lengo la makala hii si kufanya uchambuzi wa kina bali ni kuonyesha kuwa sitiari ni mbinu ya msingi ya mshairi katika kuwasilisha maana na mtazamo wake katika dhamira kadhaa. Nimeteua mashairi hayo tu ili kudhihirisha mbinu ya kisitiari katika dhamira zilizotajwa. Uchambuzi wa sitiari umezingatia mkabala wa kisemantiki unaotambua vipengele vitatu katika muundo wa sitiari: kifananishi, kitajwa na kiungo (taz. Richards 1936; Leech 1969). Hitimisho muhimu ni kwamba sitiari ni mbinu inayoyawezesha mashairi hayo kuchanuza mawazo na hisia kwa uwazi na athari nzito. / This article analyses metaphors in Kichomi, the first collection of poems by the late Euphrase Kezilahabi. The poems analysed deal with the following main themes: the meaning of life, colonial oppression, and the current state of Africa. The poems under discussion are: “Nimechoka” (I Am Tired), “Mwamba Ziwani” (Rock in Lake), “Fungueni Mlango” (Open the Door), na “Kisu Mkononi” (Knife in Hand; theme: meaning of life); “Hadithi ya Mzee” (An Old Man’s Tale) (theme: colonial oppression); “Afrika na Watu Wake” (Africa and Its People), “Kumbe” (That’s Why ), and “Namagondo” (Namagondo; theme: current state of Africa). The structure of these poems does not follow the conventional rules of metre and rhyme. The aim of this article is not a thorough analysis, but to show that metaphor is a fundamental device for the poet to present meaning and his view concerning a variety of themes. I have selected these poems only in order to make the device of metaphor clear concerning the mentioned themes. The analysis proceeds on a semantic approach which recognizes three aspects of metaphor: vehicle, tenor and ground (cf. Richards (1936); Leech (1969:153-56)). An important conclusion is that metaphor is a device which enables the poems to evoke thoughts and feelings in a candid manner and with a deep impact.

Identiferoai:union.ndltd.org:DRESDEN/oai:qucosa:de:qucosa:72136
Date14 September 2020
CreatorsKahigi, Kulikoyela K.
ContributorsUniversität Leipzig
Source SetsHochschulschriftenserver (HSSS) der SLUB Dresden
LanguageSwahili
Detected LanguageUnknown
Typeinfo:eu-repo/semantics/publishedVersion, doc-type:article, info:eu-repo/semantics/article, doc-type:Text
Rightsinfo:eu-repo/semantics/openAccess
Relation1614-2373, urn:nbn:de:bsz:15-qucosa2-721318, qucosa:72131

Page generated in 0.0026 seconds