Mabaraza na vyombo wenza vya kuendeleza lugha ya Kiswahili kwa upande wa Tanzania Bara na yale ya Tanzania Zanzibar hivi karibuni yameidhinisha kamusi za Kiswahili zinazopelekea kuwa na vielelezo anuwai vya usanifu wa lugha ya Kiswahili. Kamusi ya Kiswahili Sanifu (KKS) ya TUKI (sasa TATAKI) ya 2004 na ile ya Kamusi la Kiswahili Fasaha (KKF) ya BAKIZA ya 2010 ni ushahidi kuwa launi za Kiswahili Sanifu dhidi ya Kiswahili Fasaha zinarasimishwa. Kwa kutumia vigezo vya nadharia ya usanifishaji lugha ya Haugen (1966, 1987), makala haya yanajenga hoja kuwa tayari tumeshapata launi rasmi mbili za Kiswahili. Mapitio ya maandiko rasmi kinzani ya wasomi wa Tanzania bara na yale ya wasomi wa Zanzibar yanathibitisha kukubalika kwa launi hizo. Tahadhari kwa wahariri, walimu wa Kiswahili kama lugha ya kigeni, wanasheria, waandishi wa habari, wafasiri na watumiaji wa kawaida inatolewa juu ya kubainisha waziwazi launi hizo rasmi katika kazi zao za kila siku.
Identifer | oai:union.ndltd.org:DRESDEN/oai:qucosa:de:qucosa:11854 |
Date | 06 March 2013 |
Creators | Kipacha, Ahmad |
Contributors | The Nelson Mandela African Institute of Science and Technology, Universität Leipzig |
Source Sets | Hochschulschriftenserver (HSSS) der SLUB Dresden |
Language | Swahili |
Detected Language | Unknown |
Type | doc-type:article, info:eu-repo/semantics/article, doc-type:Text |
Source | Swahili Forum 19 (2012), S. 1-22 |
Rights | info:eu-repo/semantics/openAccess |
Relation | urn:nbn:de:bsz:15-qucosa-107567, qucosa:11865 |
Page generated in 0.0012 seconds