Return to search

Uchanganuzi wa hiponimia za vitenzi vya Kiswahili

Hiponimia ni uhusiano wa kifahiwa unaodhihirika baina ya leksimu ya jumla (hipanimu) na mahususi (hiponimu). Kama vile hipanimu mzazi hujumuisha hiponimu baba na mama. Uhusiano huu wa kihiponimia ulidhukuriwa na wanaisimu wa awali kuwa unahusisha leksimu nomino pekee. Hata hivyo, tafiti za hivi punde zinadhihirisha kuwa hiponimia huweza kudhihirika pia miongoni mwa kategoria za vivumishi, vielezi na vitenzi. Ingawa kuna midhihiriko ya hiponimia za vitenzi vya Kiswahili, wataalamu kadha wameelekea kushughulikia hiponimia za nomino na kutotilia maanani vitenzi. Hivyo basi, makala hii imechanganua uhusiano wa kihiponimia unaodhihirika miongoni mwa vitenzi teule vya Kiswahili. Katika kushughulikia suala hili, hipanimu vitenzi 24 kutoka kamusi za Kiswahili zimeteuli¬wa kimakusudi na hiponimu husika kutolewa. Nadharia ya Uchanganuzi Vijenzi kwa mujibu wa Katz na Fodor imezingatiwa katika uchanganuzi wa hiponimia hizi. Katika nadharia hii, sifa bainifu za hiponimu husika huonyeshwa kwa kutumia alama maalum za [+, -]. Data kuhusu hiponimia za vitenzi ilipekuliwa kutoka kamusi za Kiswahili kwa kuzingatia mwelekeo wa kiishara au kisintaksia kwa mujibu wa Hearst, na Snow na wenzake ili kuweza kutambua hipanimu na hiponimu husika katika sentensi. Hiponimia hizi zimechanganuliwa na kuwasilishwa kwa mtindo wa nadharia ya seti. / Hyponymy is a sense relation existing between general lexemes (hypernym) and the specific ones (hyponym). For instance, a hypernym parent includes hyponyms like father and mother. The hyponymy relation was regarded by earlier linguists that it could exist only amongst nouns. However, recent studies indicate that hyponymy can also be manifested in other categories such as adjectives, adverbs and verbs. Though there is hyponymy relation existing amongst Kiswahili verbs, various scho¬lars have tended to focus on nominal hyponymy and disregard verbal hyponymy. Therefore, this article has analyzed the hyponymy relation existing amongst selected Kiswahili verbs. In this regard, 24 verbal hypernyms from Kiswahili dictionaries were purposively sampled and their specific hyponyms indicated. Componential Analysis theory by Katz and Fodor has been used in the analysis of these hyponyms. The theory focuses on distinctive features of specific hyponyms that are normally shown by the use of specific signs [+, -]. The data on verbal hyponymy was observed from the Kiswahili dictionaries by the application of symbolic or syntactic approach propounded by Hearst, and Snow et al in order to identify the hypernyms and specific hyponyms in a sentence. These hyponymy relations are analyzed and presented using the set theory style.

Identiferoai:union.ndltd.org:DRESDEN/oai:qucosa.de:bsz:15-qucosa-220460
Date10 March 2017
CreatorsOdoyo Okal, Benard, Indede , Florence, Sangai Mohochi, Ernest
ContributorsChuo Kikuu cha Maseno, Idara ya Kiswahili na Lugha Nyingine za Kiafrika, Chuo Kikuu cha Rongo, Idara ya Lugha, Isimu na Fasihi, Universität Leipzig, Institut für Afrikanistik
PublisherUniversitätsbibliothek Leipzig
Source SetsHochschulschriftenserver (HSSS) der SLUB Dresden
LanguageSwahili (individual language)
Detected LanguageUnknown
Typedoc-type:article
Formatapplication/pdf
SourceSwahili Forum 23 (2016), S. 122-136

Page generated in 0.0025 seconds