Return to search

Siku Moja Ofisini – Nafasi ya Upapasi Mjini Zanzibar

Tukizingatia kona maalum mjini Zanzibar, yaani ofisini, mtaani Shangani Posta, leo hii mimi na mwenzangu Muchi tunataka kuwahadithia kuhusu kikundi cha vijana wanaoitwa mapapasi ambao wamekuwa wanafanya kazi katika sekta ya utalii tangu miaka ya Themanini, japo nafasi yao haijawahi kutambuliwa wala kurasimishwa na serikali. Badala yake, mara nyingi vijana hao wamekuwa wanaudhiwa, kupuuzwa na kuadhibiwa kwa vile wanapwaya kwenye dira ya kiserikali ya kuigeuza Zanzibar kuwa mahali pa kutalii (kwa maana ya touristic destination) pakiingizwa kwenye mikondo mikali ya kiliberali mamboleo. Muchi na mimi tunajadiliana na kusimulia (hi)stori(a) yenye pande zaidi ya mbili. Tutawafafanulia kazi ya upapasi kama ilivyokuwa zamani na sasa hivi. Pia, tutatafakari juu ya nafasi ya upapasi (na uwenyeji) mjini Zanzibar, tukichambua maana, athari na uwezo wake. Hivyo, tutazingatia nafasi kama kielelezo cha au methodolojia ya kuchambua maneno ya Kiswahili kama vile yalivyo, lile linaloliwezesha, pamoja na maana yao. Umbo lenyewe la mazungumzo linasisitiza kuwa fikra zinazotokea kwenye mahusiano yanazaliwa konani, pale ambapo hakuna anayetiliwa (na kinachotiliwa) maanani kabla hajapewa (na hakijapewa) nafasi huko huko, nafasi ambayo hatimaye ndiyo ya Muchi na yangu pia. / By exploring the microcosmos of a junction (kona) in the neighbourhood of Shangani Posta, in the city of Zanzibar, today Muchi and I will tell you the (hi)story of a unique segment of Zanzibari male urban youth, known as mapapasi, working in tourism since the 80s. While been neglected and denied an official, formal and legal recognition by the government, they have been continuously harassed, intimidated and shamed because perceived as not belonging, not fitting the governmental project of turning Zanzibar into a touristic destination. The following conversation aims at disclosing the complexity hidden behind the mainstream one-sided picture of them. Looking at the past and contemporary practices of upapasi, Muchi and I reflect on the nafasi of upapasi in urban Zanzibar and matter-forth upapasi (and uwenyeji as an instance of spatial il/legalization), their meaning and their doing. In this way, we are attentive to the wor(l)d nafasi, as analytical lens to get a sense – kusikia, kuona, kuwa na – urban Zanzibar. The very form of conversation is meant to think thoughts as they are co-constituted by and within the relationalites of the kona, whereas no-body is predetermined, rather every-body is co-constituted in the very situatedness in which also Muchi and I (be)come-with.

Identiferoai:union.ndltd.org:DRESDEN/oai:qucosa:de:qucosa:85803
Date05 June 2023
Creators(Mustafa Salum Abdulla), Muchi, (Irene Brunotti), Bahati
ContributorsUniversität Leipzig
Source SetsHochschulschriftenserver (HSSS) der SLUB Dresden
LanguageSwahili
Detected LanguageUnknown
Typeinfo:eu-repo/semantics/publishedVersion, doc-type:article, info:eu-repo/semantics/article, doc-type:Text
Rightsinfo:eu-repo/semantics/openAccess
Relation1614-2373, urn:nbn:de:bsz:15-qucosa2-857753, qucosa:85775

Page generated in 0.0015 seconds