Nyimbo, kama tanzu ya fasihi yeyote ile zina majukumu mbalimbali
ambayo hutekeleza katika jamii. Lengo kuu la fasihi ni lile la kuielimisha
na hata kuiburudisha jamii. Ndivyo ilivyo katika nyimbo kwa sababu
kupitia kwazo wanajamii huburudika na kuelimishwa. Ni kwa sababu
hiyo ndipo makala hii inalenga kuangalia nafasi ya nyimbo
zinazopendwa katika fasihi ya Kiswahili. Huu ni utanzu ambao
huwafikia watu wengi katika jamii. Kutokana na kutumia lugha ya
Kiswahili, utanzu huu unaweza kueleweka na Wakenya wengi. Nchini
Kenya, vyombo vya habari vimeipa fasihi hii nafasi kubwa sana na hivyo
basi kuipanua hadhira yake. Hii ni kutokana na sababu kuwa fasihi hii
inathaminiwa sana na wengi na ipewe nafasi kubwa katika vyombo vya
habari hasa katika redio kwa muda mrefu. Ni kutokana na sababu hii
ndipo tunajaribu kuonyesha nafasi yake katika fasihi ya Kiswahili.
Identifer | oai:union.ndltd.org:DRESDEN/oai:qucosa:de:qucosa:11720 |
Date | 30 November 2012 |
Creators | Ngugi, Pamela M. Y. |
Contributors | Kenyatta University, Universität zu Köln |
Source Sets | Hochschulschriftenserver (HSSS) der SLUB Dresden |
Language | Swahili |
Detected Language | Unknown |
Type | doc-type:article, info:eu-repo/semantics/article, doc-type:Text |
Source | Swahili Forum; 7(2000), S. 145-152 |
Rights | info:eu-repo/semantics/openAccess |
Relation | urn:nbn:de:bsz:15-qucosa-93696, qucosa:11587 |
Page generated in 0.0018 seconds