Return to search

Methali za Kiswahili zihusuzo ulemavu: mitazamo na athari zake katika jamii

Methali ni kipera muhimu cha fasihi simulizi katika kutoa mafunzo kutokana na maudhui yapatikanayo humo. Zimekuwa zikichukuliwa kuwa zina ukweli, hekima na busara kwa jamii husika. Lengo la makala hii ni kuzihakiki methali za Kiswahili ambazo zinahusu ulemavu ili kuelewa mitazamo iliyomo katika methali hizo na athari zake katika jamii. Maswali tunayojibu ni: Je, methali hizo zinabeba mitazamo gani ya jamii? Nini nafasi na athari ya mitazamo hiyo kwa maendeleo endelevu ya watu wenye ulemavu na jamii husika? Data za makala hii zimekusanywa kupitia usomaji wa maandiko mbalimbali maktabani na kufanya mahojiano na wanajamii. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa, methali zimebeba mitazamo hasi na chanya kuhusu ulemavu na watu wenye ulemavu katika jamii. Aidha, methali hizo zinazungumzia mambo yanayohusu si tu ulemavu bali pia zinabeba mitazamo anuwai na falsafa ya Kiafrika kuhusu mambo mbalimbali katika jamii. Vilevile, imebainika kuwa methali hizo zinajenga na kuendeleza unyanyapaa na usaguzi kwa watu wenye ulemavu na hata makundi mengine katika jamii. Makala pia imebaini kuwa pamoja na ukweli kwamba methali zimekuwa chombo muhimu cha kupitishia falsafa na mafunzo mbalimbali kwa maendeleo ya jamii, baadhi ya methali hizo zinapaswa kufanyiwa marekebisho ili kuakisi mabadiliko ya kimtazamo na maendeleo mbalimbali katika wakati wa sasa.

Identiferoai:union.ndltd.org:DRESDEN/oai:qucosa:de:qucosa:80618
Date12 September 2022
CreatorsMchepange, Shani Omari, Mahenge, Elizabeth Godwin
ContributorsUniversität Leipzig
Source SetsHochschulschriftenserver (HSSS) der SLUB Dresden
LanguageSwahili
Detected LanguageUnknown
Typeinfo:eu-repo/semantics/publishedVersion, doc-type:article, info:eu-repo/semantics/article, doc-type:Text
Rightsinfo:eu-repo/semantics/openAccess
Relation1614-2373, urn:nbn:de:bsz:15-qucosa2-806124, qucosa:80612

Page generated in 0.002 seconds