Return to search

Kasida ya Hamziyyah (part 1)

Kasida ya Hamziyyah, yumkini, ndiyo tafsiri ya Kiswahili ya zamani zaidi.
Kiswahili kilichotumiwa katika ukawafi huu kimechakaa sana hata
maneno mengine hayatumiki tena. Hii ni kasida ambayo ni maarufu
sana katika ulimwengu wa fasihi na dini ya Kiislamu na Waswahili
huikariri wakati wa sherehe za Maulidi ya Nabii Muhammadi au
wanapocheza Twari la Ndiya. Kasida hii ya Hamziyah pia hujulikana
kama Chuo cha Hamziyah au Utenzi wa Hamziyah. Kasida ya
Hamziyyah ilitafsiriwa kutoka kwa Kiarabu na Sayyid Aidarus bin
Athumani bin Sheikh Abubakar bin Salim hapo mwaka wa 1652b.
Pamoja na kuinukuu kwa hati za Kirumi nimebawibu Hamziyah katika
sehemu mbalimbali, kulingana na maudhui yake, ili iweze kusomeka
kwa urahisi na iweze kuwavutia wasomaji. Katika miswada ya Kiswahili
niliyoipata, mswada mmoja una ubeti mmoja zaidi.

Identiferoai:union.ndltd.org:DRESDEN/oai:qucosa:de:qucosa:11721
Date30 November 2012
CreatorsMutiso, Kineene Wa
ContributorsUniversity of Nairobi, Universität zu Köln
Source SetsHochschulschriftenserver (HSSS) der SLUB Dresden
LanguageSwahili
Detected LanguageUnknown
Typedoc-type:article, info:eu-repo/semantics/article, doc-type:Text
SourceSwahili Forum; 8(2001), S. 81-115
Rightsinfo:eu-repo/semantics/openAccess
Relationurn:nbn:de:bsz:15-qucosa-93705, qucosa:11588

Page generated in 0.002 seconds