Dhana ya usarufishaji, kama Kamusi ya Isimu na Lugha inavyoeleza, ni ubadilishaji wa neno huru ama mofimu huru yenye maana ya kisemantiki na kuifanya mofimu funge na yenye maana ya kisarufi zaidi.
Tunaposema kuhusu usarufishaji, mara nyingi tunamaanisha hasa
ubadilishaji wa neno huru liwe mofimu. Miongoni mwa aina zote za maneno, ambazo zinaweza kusarufishwa, zile zinazotumika mara nyingi zaidi ni nomino na vitenzi. Ningetaka kujibu swali juu ya kazi ya kisarufi ya leksimu mwana: baada ya kuzichunguza maana zake za kisarufi inawezekana kutilia mkazo kwamba katika lugha ya Kiswahili tunashuhudia mwanzo wa kuibadilisha nomino huru mwana iwe kiambishi awali cha uundaji wa maneno mapya yanayotaja watu mbalimbali kutokana na kazi, shughuli zao, kuwepo katika vyama n.k. Inawezekana kwamba maneno ambatani yanayoanzia na mwana
yanaunda ngeli maalum ya nomino (sawa na ngeli ya 1a/2a ya lugha
nyingine za Kibantu).
Identifer | oai:union.ndltd.org:DRESDEN/oai:qucosa.de:bsz:15-qucosa-98181 |
Date | 30 November 2012 |
Creators | Gromova, Nelli V. |
Contributors | Moscow State Lomonosov University, Institute of Asian and African Studies, Universität zu Köln, Institut für Afrikanistik |
Publisher | Universitätsbibliothek Leipzig |
Source Sets | Hochschulschriftenserver (HSSS) der SLUB Dresden |
Language | Swahili (individual language) |
Detected Language | Unknown |
Type | doc-type:article |
Format | application/pdf |
Source | Swahili Forum; 8(2001), S. 59-65 |
Page generated in 0.0022 seconds