Mwanadamu amejaribu kwa vyovyote vile kuvumbua na kunyumbua mambo mapya ambayo yataleta mvuto na kupimia akili yake kiubunifu katika hali ya kutaka kutangamana zaidi na binadamu mwenzake au kutaka kuelewa zaidi ulimwengu wake. Ndiposa washairi wengi wa kisasa wanashikilia kwamba ulimwengu unabadilika na hivyo utamaduni wa ushairi lazima ubadilike. Katika wasilisho hili tunajadili mabadiliko haya ya kimaumbo na athari zake katika ushairi wa Kiswahili. Si lengo letu kushawishi msomaji kujiunga na kikundi fulani cha ushairi bali kuangazia hoja mwafaka zinazotokana na mivutano na mikinzano katika mabadiliko haya, na namna mitazamo hii inavyofanikisha maendeleo ya ushairi.
Identifer | oai:union.ndltd.org:DRESDEN/oai:qucosa:de:qucosa:10689 |
Date | 03 December 2012 |
Creators | Indede, Florence Ngesa |
Contributors | Maseno University, Universität Mainz |
Source Sets | Hochschulschriftenserver (HSSS) der SLUB Dresden |
Language | Swahili |
Detected Language | Unknown |
Type | doc-type:article, info:eu-repo/semantics/article, doc-type:Text |
Source | Swahili Forum; 15(2008), S. 73-94 |
Rights | info:eu-repo/semantics/openAccess |
Relation | urn:nbn:de:bsz:15-qucosa-94062, qucosa:11593 |
Page generated in 0.0021 seconds