Return to search

Mwanamke angali tata katika ushairi wa kisasa?

Sanaa ya ushairi inajisawiri kama nyenzo muhimu katika maendeleo na ukuaji wa binadamu ulimwenguni. Ujenzi wa taswira zinazowasilisha mada nyeti za kijamii ni changamoto ya kiusanii inayoibua maswala tata. Ndiposa wasilisho hili linachunguza mjadala wa usawiri wa mwanamke katika ushairi wa kisasa. Mada nyingi zinazohakiki matini za kishairi hulenga miuundo, mitindo na maswala mengineyo ya kijamii bila kuangazia swala la utata wa mwanamke. Uzingatifu wa vipengee hivi umefifisha uangafu wa taswira ya mwanamke katika ushairi wa Kiswahili kana kwamba ushairi umempuuza mwanamke kama mhusika mkuu. Tunachukulia kwamba matini za kishairi za kisasa zinahusisha mbinu na nyenzo mpya ambazo zimebadilisha sura na taswira ya mwanamke. Maswali yanayoibuka ni; Je, Mwanamke angali tata katika ushairi wa kisasa kwenye enzi ya karne ya ishirini na moja? Je, umbo jipya la mwanamke ni lipi katika ushairi wa kisasa?

Identiferoai:union.ndltd.org:DRESDEN/oai:qucosa:de:qucosa:11743
Date03 December 2012
CreatorsIndede, Florence
ContributorsChuo Kikuu cha Maseno, Universität Mainz
Source SetsHochschulschriftenserver (HSSS) der SLUB Dresden
LanguageSwahili
Detected LanguageUnknown
Typedoc-type:article, info:eu-repo/semantics/article, doc-type:Text
SourceSwahili Forum; 18(2011), S. 163-197
Rightsinfo:eu-repo/semantics/openAccess
Relationurn:nbn:de:bsz:15-qucosa-94462, qucosa:11600

Page generated in 0.002 seconds