• Refine Query
  • Source
  • Publication year
  • to
  • Language
  • 21
  • 9
  • 1
  • 1
  • Tagged with
  • 32
  • 32
  • 11
  • 11
  • 11
  • 11
  • 11
  • 9
  • 7
  • 7
  • 6
  • 5
  • 5
  • 4
  • 4
  • About
  • The Global ETD Search service is a free service for researchers to find electronic theses and dissertations. This service is provided by the Networked Digital Library of Theses and Dissertations.
    Our metadata is collected from universities around the world. If you manage a university/consortium/country archive and want to be added, details can be found on the NDLTD website.
21

Mgullu, Richard S. 1999. Mtalaa wa isimu: fonetiki, fonolojia na mofolojia ya kiswahili. Nairobi: Longhorn Publishers. Kurasa xv, 247.

Ngonyani, Deogratias 30 November 2012 (has links)
Kitabu hiki kinaleta matumaini makubwa ya kuwawezesha wengi ku-soma juu ya lugha yao na kuamsha hamasa ya kujifunza zaidi juu ya lugha hii tukufu na lugha nyingine za kiafrika.
22

Matatizo ya matumizi ya lugha katika vyombo vya habari: mifano kutoka Kenya

King´ei, Geoffrey Kitula 30 November 2012 (has links)
Lugha inaweza kutumiwa kwa njia ya ubunifu wenye ufasaha ufaao ili kuwasiliana au pia ikatumiwa visivyo na kwa njia potovu. Ni nini hasa maana ya kutumia lugha kwa njia potovu? Pengine ni rahisi kueleza kinyume chake. Mtumiaji wa lugha mwenye ubunifu huzingatia rasimali zote za lugha. Mwandishi maarufu wa fasihi barani Afrika, Chinua Achebe, huitumia lugha kama kituo kilicho hai na pia kuendelea. Katika juhudi za kuifanya lugha kumwezesha kutoa maoni, maelekezo, habari na hisia, mtumiaji kama huyu hutambua kuwa lugha ikitumiwa ipasavyo huleta uhai katika taaluma ya mawasiliano. (Luvai, 1991: 60) Hata hivyo, katika Kenya, kiwango che ubora wa uandishi kwa jumla kimeshuka sana katika miaka ishirini iliyopita. Makala hii itachunguza kwa muhtasari ushahidi wa matumizi yasiyofaa ya lugha ya Kiswahili katika vyombo vya habari km. redio, televisheni na magazeti.
23

Hali ya kutatanisha ya Kiswahili hivi leo Afrika ya Mashariki

Sengo, Tigiti Shaaban Yusuf 30 November 2012 (has links)
The essay critically discusses the confusing state of the various Swahili language policies and studies brought forth in the colonial and post-colonial periods and examines the historical factors of the diversity within the Swahili language, which was once confined to the coastal area and later spread to the present area of distribution. The discussion focusses on the construction of Standard Swahili and the status of Swahili in regard to other East African languages. Special criticism is raised against recent East African and other authors, who wrote on the apparent unity of the Swahili language which they see as a result of the modern Tanzanian language policy.
24

Ufundishaji wa kiswahili Marekani: maendeleo na changamoto

WaNjogu, John Kiarie 03 December 2012 (has links)
Kiswahili ni mojawapo ya lugha za Kiafrika zinazofundishwa nchini Marekani. Baada ya Vita Baridi kuisha na kuvunjika kwa muungano wa Sovieti, Marekani ilihimiza lugha fulani zifundishwe kwa maslahi ya mahitaji yake ya kiuchumi na usalama. Kutokana na kuanzishwa kwa lugha za Kiafrika katika elimu ya juu, vyuo vinavyofundisha lugha ya Kiswahili Marekani vimeongezaka kufikia zaidi ya hamsini. Katika makala hii tutaelezea ufundishaji wa lugha ya Kiswahili, utayarishaji wa walimu na vifaa, na matatizo yanayokumba ufundishaji wa Kiswahili (na lugha zingine za Kiafrika kwa jumla) kama lugha ya kigeni. Mwisho tutapendekeza njia za kusuluhisha kwa matatizo haya.
25

Taasisi ya Nchi za Asia na Afrika, Chuo Kikuu cha Moscow. Uchunguzi wa Kiswahili katika Urusi

Gromova, Nelly V. 03 December 2012 (has links)
Utafiti wa lugha ya Kiswahili katika Urusi ulianza mwishoni mwa karne ya 18. Lakini utafiti hasa wa lugha za Kiafrika katika Urusi ulihusu ukoo wa Kisemetiki. Lakini uchunguzi kamili wa lugha za Kiafrika hasa lugha hai ulianza katika Urusi baada ya Mapinduzi ya Oktoba yatokee. Na lugha ya kwanza ya Afrika ya kitropiki iliyofundishwa katika Urusi ya kisoviet ilikuwa ni lugha ya Kiswahili.
26

Utegemezi au utegemeano baina ya Kenya na Tanzania katika ukuzaji na uendelezaji wa Kiswahili nchini Kenya?

Oyori Ogechi, Nathan 14 December 2012 (has links)
Makala haya yanatathmini iwapo ukuzaji na uendelezaji wa Kiswahili nchini Kenya unategemea shughuli za kuiendeleza lugha hii zinazofanywa na Tanzania ama unatokana na kutegemeana baina ya mataifa haya katika kukikuza na kukiendeleza Kiswahili. Baadhi ya njia za kuiendeleza lugha zinajumuisha: kuisanifisha, kuifanyia utafiti na kuiimarisha kwa kuitungia kamusi, vitabu vya sarufi, kazi za kisanaa na kuitumia serikalini, mahakamani, katika elimu n.k. Makala haya yanaonyesha kuwa ingawa kuna utegemeano kati ya Kenya na Tanzania katika ukuzaji na uendelezaji wa Kiswahili, Tanzania inategemewa zaidi. Hususan inadhahirishwa kuwa Kenya imeitegemea Tanzania kwa kuagizia machapisho, wataalamu wa Kiswahili mbali na kutumia istilahi na hata kuchuma nafuu mifano ya Tanzania katika utumishi wa umma. Fauka ya hayo, inaonyeshwa kuwa pale ambapo Kenya haijafaidi kutokana na ufanisi wa Tanzania, ikiiga mfano wa Tanzania, upo uwezekano wa kufaulu.
27

Nafasi ya Kiswahili katika ujenzi wa jamii mpya ya Afrika Mashariki

G. Kiango, John 14 December 2012 (has links)
Lugha ni chombo muhimu sana cha mawasiliano kilichoundwa na sauti za nasibu za kusemwa na kutumiwa na jamii ya utamaduni fulani. Jinsi ambavyo zipo jamii nyingi za tamaduni mbalimbali duniani, vivyo hivyo ziko lugha mbalimbali zilizoundwa kukidhi haja ya mawasiliano ya tamaduni mbalimbali. Maingiliano ya jamii zenye tamaduni na lugha mbalimbali yanayotokana na mashirikiano katika shughuli za biashara na nyinginezo za kijamii, huzusha haja ya kuwepo kwa lugha moja itakayoweza kuwaungaanisha watu hao wenye tamaduni na lugha mbalimbali. Maingiliano kama hayo yanaweza kuwa katika viwango mbalimbali.
28

An analysis of the socio-pragmatic motivations for code-switching in Rwanda

Habyarimana, Heli 09 1900 (has links)
Text in English / The study examines the social motivations that prompt the Rwandan bilingual speakers to code-switch from Kinyarwanda to English, French or Kiswahili in their casual conversations about real-life situations. Methodological techniques used for data collection are ethnographic non-participant observation, oral interviews, focus group discussions and shorthand notes techniques. Examples were examined and interpreted within Myers-Scotton’s Markedness Model as the main theoretical framework for the study. The research findings align with Myers-Scotton’s categories such as the sequential unmarked choice, code-switching itself as the unmarked choice, the marked choice and the exploratory choice respectively. The main social factors that influence code-switching among the Rwandan bilingual speakers were identified as signalling educated status, expressing different social identities, demonstrating measures of power, authority and prestige, narrowing or widening social distance, and maintaining relationships. These results support the hypothesis that code-switching is a strategy to maximise social benefits from the interlocutors in conversation. / Linguistics and Modern Languages / M.A. (Sociolinguistics)
29

Ujuzi wa watoto/vijana katika simulizi za maisha

Schulz-Burgdorf, Ulrich 14 December 2012 (has links)
Kutoka elimu ya lugha tunajua kwamba kila mtu aliyenena ana ujuzi maalum - kama John Lyons alivyoeleza katika kitabu chake Language and Linguistics (1981), katika sura kuhusu lugha na utamaduni wa wasemaji. Lyons anatueleza kwamba kila mtu hushika ujuzi huo kwa njia ya kufunzwa lugha na huutumia ujuzi, huuongeza na huubadilisha kwa muda wa maisha yake yote; ni jinsi yake ya kujua mambo ya ulimwengu. Katika maelezo yafuatayo napenda kuonyesha ujuzi uliomo katika habari nilizopewa na kijana, jina lake ni Timothy Lawrence ambaye alikuwa na umri wa kumi na tatu siku zile. Ujuzi wake ni juu ya maisha yake ya kipokomo na pia ni ujuzi wa kumweleza mgeni mambo hayo - yaani ujuzi au uwezo wa kuzisimulia habari hizo. Habari zake zinatuonyesha vizuri simulizi ya maisha ya binafsi (au autobiographical narrative) ni nini, yenye ujuzi gani na jinsi gani ya kutazama maisha kwa macho ya mwenyeji kijana.
30

Kutoka lugha kienzo hadi lugha ya isimu: matatizo yanayotinga kiswahili kama lugha ya kufunzia isimu vyuoni vikuu nchini Kenya

Mbatha Mathooko, Petronilla 14 December 2012 (has links)
Makala hii inachunguza hali ya somo la isimu ya lugha linalofundishwa katika nyingi ya idara za Kiswahili vyuoni vikuu nchini Kenya. Inaangazia matatizo yanayotinga kufana kwa somo hili. Inahitimiza kwa kupendekeza kwamba iwapo matokeo mazuri yatapatikana na wanafunzi wa somo hili, yafaa matatizo yanayokwamiza somo hili yatatuliwe, hasa kwa upande wa usawazishaji wa istilahi, tafsiri, uzito wa kozi na mengineyo. Makala hii inapendekeza kuwa ni muhimu kila chuo kikuu kiunde kamati ya kuchunguza jambo hili.

Page generated in 0.052 seconds