Sarufi inafafanuliwa kama kanuni, sheria au taratibu zinazotawala katika viwango vyote vya uchambuzi wa lugha ambavyo ni umbosauti (au fonolojia), umboneno (au mofolojia), miundomaneno (au sintaksia) na umbomaana (au semantiki). Kuhusiana na masuala ya tafsiri, kanuni muhimu sana zinazopaswa kuzingatiwa ni zile za kiwango cha miundomaneno au sentensi. Kanuni katika kiwango cha miundomaneno, kwa jumla, huwa zinahusu uchaguzi wa maneno sahihi katika muktadha wa maelezo na jinsi maneno kama hayo yanavyopangiliwa kuunda vipashio mbalimbali vya sentensi na sentensi zenyewe. Kwa jumla, huwa kuna aina mbili za tafsiri: tafsiri halisi na tafsiri huru. Nasution 1988 hufikiri kwamba aina hizi mbili za tafsiri hukinzana.
Identifer | oai:union.ndltd.org:DRESDEN/oai:qucosa.de:bsz:15-qucosa-98293 |
Date | 30 November 2012 |
Creators | Kihore, Yared M. |
Contributors | University of Dar es Salaam, Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Universität Mainz, Insitut für Ethnologie und Afrikastudien |
Publisher | Universitätsbibliothek Leipzig |
Source Sets | Hochschulschriftenserver (HSSS) der SLUB Dresden |
Language | Swahili (individual language) |
Detected Language | Unknown |
Type | doc-type:article |
Format | application/pdf |
Source | Swahili Forum; 12(2005), S. 109-120 |
Page generated in 0.0019 seconds