Return to search

Mielekeo ya wasomi wa Kiswahili na viongozi wa Afrika Mashariki kuhusu lugha ya Kiswahili / The attitude of Swahili intellectuals and East-African leaders towards the language of Kiswahili

Lugha ya Kiswahili imeenea na kukua kiasi cha kuweza kupambana na zingine katika ngazi za kimataifa kwenye mfumo wa sasa wa utandawazi. Hata hivyo, Kiswahili hakiwezi kupata fanaka inayotarajiwa huko nje iwapo hakithaminiwi na kudhaminiwa nyumbani (Afrika Mashariki). Bado lugha ya Kiswahili inakumbana na pingamizi nyingi mno; na miongoni mwa vikwazo hivyo ni mielekeo ya lugha inayobainika katika jamii. Makala hii inajikita zaidi katika mielekeo ya viongozi wa Afrika Mashariki, na wasomi wa Kiswahili kuhusu nafasi na umuhimu wa Kiswahili. Viongozi na wasomi wana ushawishi mkubwa sana kutokana na nafasi yao katika jamii. Wote wanaheshimika na kuenziwa; viongozi kutokana na mamlaka waliyopewa, na wasomi kwa sababu ya maarifa waliyonayo. Kutokana na ukweli huo, tabia na mienendo yao, pamoja na matamko yao mbalimbali yana athari kubwa sana katika jamii. Mara nyingi, watu wengi hupenda kuiga wayafanyayo; hali inayobainika pia katika matumizi ya lugha. Kabla ya kuijadili mielekeo na matumizi yao ya lugha, maswala mawili muhimu yanayochangia ujenzi wa hiyo mielekeo katika jamii yatazungumziwa: thamani ya lugha, na zoezi la kujifunza lugha ya pili.

Identiferoai:union.ndltd.org:DRESDEN/oai:qucosa:de:qucosa:11464
Date January 2011
CreatorsMohochi, Sangai
ContributorsStanford University, Universität Mainz
Source SetsHochschulschriftenserver (HSSS) der SLUB Dresden
LanguageEnglish
Detected LanguageUnknown
Typedoc-type:article, info:eu-repo/semantics/article, doc-type:Text
SourceSwahili Forum 18 (2011), S. 24-36
Rightsinfo:eu-repo/semantics/openAccess
Relationurn:nbn:de:bsz:15-qucosa-94462, qucosa:11600

Page generated in 0.0017 seconds