Return to search

Ufundishaji wa kiswahili Marekani: maendeleo na changamoto

Kiswahili ni mojawapo ya lugha za Kiafrika zinazofundishwa nchini Marekani. Baada ya Vita Baridi kuisha na kuvunjika kwa muungano wa Sovieti, Marekani ilihimiza lugha fulani zifundishwe kwa maslahi ya mahitaji yake ya kiuchumi na usalama. Kutokana na kuanzishwa kwa lugha za Kiafrika katika elimu ya juu, vyuo vinavyofundisha lugha ya Kiswahili Marekani vimeongezaka kufikia zaidi ya hamsini. Katika makala hii tutaelezea ufundishaji wa lugha ya Kiswahili, utayarishaji wa walimu na vifaa, na matatizo yanayokumba ufundishaji wa Kiswahili (na lugha zingine za Kiafrika kwa jumla) kama lugha ya kigeni. Mwisho tutapendekeza njia za kusuluhisha kwa matatizo haya.

Identiferoai:union.ndltd.org:DRESDEN/oai:qucosa:de:qucosa:11738
Date03 December 2012
CreatorsWaNjogu, John Kiarie
ContributorsYale University, Universität Mainz
Source SetsHochschulschriftenserver (HSSS) der SLUB Dresden
LanguageSwahili
Detected LanguageUnknown
Typedoc-type:article, info:eu-repo/semantics/article, doc-type:Text
SourceSwahili Forum; 15(2008), S. 121-133
Rightsinfo:eu-repo/semantics/openAccess
Relationurn:nbn:de:bsz:15-qucosa-94135, qucosa:11596

Page generated in 0.0014 seconds