Lugha inaweza kutumiwa kwa njia ya ubunifu wenye ufasaha ufaao ili kuwasiliana au pia ikatumiwa visivyo na kwa njia potovu. Ni nini hasa maana ya kutumia lugha kwa njia potovu? Pengine ni rahisi kueleza kinyume chake. Mtumiaji wa lugha mwenye ubunifu huzingatia rasimali zote za lugha. Mwandishi maarufu wa fasihi barani Afrika, Chinua Achebe, huitumia lugha kama kituo kilicho hai na pia kuendelea. Katika juhudi za kuifanya lugha kumwezesha kutoa maoni, maelekezo, habari na hisia, mtumiaji kama huyu hutambua kuwa lugha ikitumiwa ipasavyo huleta uhai katika taaluma ya mawasiliano. (Luvai, 1991: 60) Hata hivyo, katika Kenya, kiwango che ubora wa uandishi kwa jumla kimeshuka sana katika miaka ishirini iliyopita. Makala hii itachunguza kwa muhtasari ushahidi wa matumizi yasiyofaa ya lugha ya Kiswahili katika vyombo vya habari km. redio, televisheni na magazeti.
Identifer | oai:union.ndltd.org:DRESDEN/oai:qucosa.de:bsz:15-qucosa-97905 |
Date | 30 November 2012 |
Creators | King´ei, Geoffrey Kitula |
Contributors | Kenyatta University, Department of Kiswahili and African Languages, Universität zu Köln, Institut für Afrikanistik |
Publisher | Universitätsbibliothek Leipzig |
Source Sets | Hochschulschriftenserver (HSSS) der SLUB Dresden |
Language | Swahili (individual language) |
Detected Language | Unknown |
Type | doc-type:article |
Format | application/pdf |
Source | Swahili Forum; 7(2000), S. 45-56 |
Page generated in 0.0022 seconds