Return to search

Uzingatifu wa sarufi katika tafsiri

Sarufi inafafanuliwa kama kanuni, sheria au taratibu zinazotawala katika viwango vyote vya uchambuzi wa lugha ambavyo ni umbosauti (au fonolojia), umboneno (au mofolojia), miundomaneno (au sintaksia) na umbomaana (au semantiki). Kuhusiana na masuala ya tafsiri, kanuni muhimu sana zinazopaswa kuzingatiwa ni zile za kiwango cha miundomaneno au sentensi. Kanuni katika kiwango cha miundomaneno, kwa jumla, huwa zinahusu uchaguzi wa maneno sahihi katika muktadha wa maelezo na jinsi maneno kama hayo yanavyopangiliwa kuunda vipashio mbalimbali vya sentensi na sentensi zenyewe. Kwa jumla, huwa kuna aina mbili za tafsiri: tafsiri halisi na tafsiri huru. Nasution 1988 hufikiri kwamba aina hizi mbili za tafsiri hukinzana.

Identiferoai:union.ndltd.org:DRESDEN/oai:qucosa.de:bsz:15-qucosa-98293
Date30 November 2012
CreatorsKihore, Yared M.
ContributorsUniversity of Dar es Salaam, Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Universität Mainz, Insitut für Ethnologie und Afrikastudien
PublisherUniversitätsbibliothek Leipzig
Source SetsHochschulschriftenserver (HSSS) der SLUB Dresden
LanguageSwahili (individual language)
Detected LanguageUnknown
Typedoc-type:article
Formatapplication/pdf
SourceSwahili Forum; 12(2005), S. 109-120

Page generated in 0.0025 seconds