Makala haya yanalenga kuchambua fani na maudhui, muundo na dhamira za tamthilia za Kiswahili zihusuzo VVU/UKIMWI, hasa tamthilia kutoka Tanzania, na uhusiano baina ya VVU/UKIMWI na mila za jadi kama sherehe za jando na unyago. Dhamira muhimu ya kujadili ugonjwa katika kazi za fasihi barani Afrika ilichimbuka katika sanaa za maonyesho ya jadi ya Kiafrika yaani katika shughuli za ngoma na miviga ya kidini kama matambiko kwa miungu, kumtolea Mungu kafara ili mgonjwa apate dawa au kupona. Maudhui yanayohusu ugonjwa yameingia katika tamthilia mamboleo kwa nia ya kuoanisha tamthilia ya kigeni na ngoma ya kijadi, hasa baada ya miaka ya 1980 (ling. Mlama 1983; Hussein 1983). Katika tamthilia za Tanzania za kisasa magonjwa yanayozungumziwa ni mengi, lakini kuanzia miaka ya themanini ugonjwa mpya, yaani VVU/UKIMWI, unachukua nafasi ya dhamira kuu katika kazi nyingi. Lengo kuu la makala haya ni kuchambua na kuhakiki tamthilia teule sita zihusuzo VVU/UKIMWI na kuandikwa zote na waandishi wa kutoka Tanzania. Ninachambua vipengele mbalimbali vya fani na maudhui nikiangalia uhusiano baina ya sifa za kimapokeo na za mamboleo. Ninafafanua pia athari za kimagharibi kutoka tamthilia ya Wayunani yaani vigezo vya Aristotle na dhana ya tanzia. Kwa kuunganisha nadharia za kale za Kimagharibi na za kisasa kutoka Afrika Mashariki, nitatumia pia nadharia ya korasi (Mutembei 2012), na vilevile kuchambua athari za ki-Brecht yaani ukengeushi ambazo zimekuwa na umuhimu mkubwa kwa tamthilia ya kutoka nchini kwingi Afrika na ulimwenguni kote.
Identifer | oai:union.ndltd.org:DRESDEN/oai:qucosa.de:bsz:15-qucosa-220452 |
Date | 10 March 2017 |
Creators | Nicolini, Cristina |
Contributors | University of Naples,, LUISS University of Rome,, Universität Leipzig, Institut für Afrikanistik |
Publisher | Universitätsbibliothek Leipzig |
Source Sets | Hochschulschriftenserver (HSSS) der SLUB Dresden |
Language | Swahili (individual language) |
Detected Language | Unknown |
Type | doc-type:article |
Format | application/pdf |
Source | Swahili Forum 23 (2016), S. 98-121 |
Page generated in 0.0022 seconds