• Refine Query
  • Source
  • Publication year
  • to
  • Language
  • 5
  • 2
  • 2
  • Tagged with
  • 5
  • 5
  • 5
  • 5
  • 5
  • 4
  • 4
  • 3
  • 3
  • 3
  • 3
  • 2
  • 2
  • 2
  • 2
  • About
  • The Global ETD Search service is a free service for researchers to find electronic theses and dissertations. This service is provided by the Networked Digital Library of Theses and Dissertations.
    Our metadata is collected from universities around the world. If you manage a university/consortium/country archive and want to be added, details can be found on the NDLTD website.
1

Uhakiki wa tamthilia za kiswahili zihusuzo VVU/UKIMWI

Nicolini, Cristina 10 March 2017 (has links) (PDF)
Makala haya yanalenga kuchambua fani na maudhui, muundo na dhamira za tamthilia za Kiswahili zihusuzo VVU/UKIMWI, hasa tamthilia kutoka Tanzania, na uhusiano baina ya VVU/UKIMWI na mila za jadi kama sherehe za jando na unyago. Dhamira muhimu ya kujadili ugonjwa katika kazi za fasihi barani Afrika ilichimbuka katika sanaa za maonyesho ya jadi ya Kiafrika yaani katika shughuli za ngoma na miviga ya kidini kama matambiko kwa miungu, kumtolea Mungu kafara ili mgonjwa apate dawa au kupona. Maudhui yanayohusu ugonjwa yameingia katika tamthilia mamboleo kwa nia ya kuoanisha tamthilia ya kigeni na ngoma ya kijadi, hasa baada ya miaka ya 1980 (ling. Mlama 1983; Hussein 1983). Katika tamthilia za Tanzania za kisasa magonjwa yanayozungumziwa ni mengi, lakini kuanzia miaka ya themanini ugonjwa mpya, yaani VVU/UKIMWI, unachukua nafasi ya dhamira kuu katika kazi nyingi. Lengo kuu la makala haya ni kuchambua na kuhakiki tamthilia teule sita zihusuzo VVU/UKIMWI na kuandikwa zote na waandishi wa kutoka Tanzania. Ninachambua vipengele mbalimbali vya fani na maudhui nikiangalia uhusiano baina ya sifa za kimapokeo na za mamboleo. Ninafafanua pia athari za kimagharibi kutoka tamthilia ya Wayunani yaani vigezo vya Aristotle na dhana ya tanzia. Kwa kuunganisha nadharia za kale za Kimagharibi na za kisasa kutoka Afrika Mashariki, nitatumia pia nadharia ya korasi (Mutembei 2012), na vilevile kuchambua athari za ki-Brecht yaani ukengeushi ambazo zimekuwa na umuhimu mkubwa kwa tamthilia ya kutoka nchini kwingi Afrika na ulimwenguni kote.
2

Usimulizi katika tamthilia za Kithaka wa Mberia

Njeri Waweru, Grace 10 March 2017 (has links)
Makala haya yanachunguza mtindo wa usimulizi katika tamthilia za Kithaka wa Mberia na kutoa ufafanuzi wake. Tamthilia zenyewe ni Natala (1997), Kifo Kisimani (Death at the Well, 2001) na Maua Kwenye Jua la Asubuhi (Flowers in the Morning Sun, 2004). Vipera vya usimulizi vinavyo-chunguzwa ni methali, nyimbo/ngoma, sauti na hadithi. Usimulizi ni mbinu ya fasihi simulizi iliyo na jadi ndefu. Kutokana na msingi huu, wa Mberia alioanisha usimulizi na ujumbe wa tamthilia zake ana¬powasawiri wahusika wake kupitia matendo yao na mazungumzo yao jukwaani. Umuhimu wa matu¬mizi ya mbinu ya usimulizi katika tamthilia teule unaonekana kupuuzwa na wahakiki wengi. Kwa hivyo, madhumuni ya makala haya ni kuangazia umuhimu wa usimulizi katika usawiri wa maudhui mbalimbali na kuthibitisha kuweko kwa matumizi ya usimulizi katika tamthilia teule. Ni makala ambayo yatawafaidi wanafunzi katika vyuo vinavyotoa masomo ya fasihi. Makala haya yanamdhihi¬risha wa Mberia kama mtunzi shupavu, anayeteka makini ya hadhira yake kwa kuiwezesha kutafakari zaidi kuhusu masuala anayojadilia tamthiliani, kwa matumizi ya usimulizi. / This paper analyses narrative style in Kithaka wa Mberia’s plays. The plays analysed are Natala (1997), Kifo Kisimani (Death at the Well, 2001) na Maua Kwenye Jua la Asubuhi (Flowers in the Morning Sun, 2004). The elements of narrative style analysed are proverbs, songs/dances, voice and epic. Narrative style has a long history in oral literature. It has been integrated into written literature and thus lost its initial outlook which had led to its disregard by many analysts in the past. The objectives of this essay are to discuss narrative style in the selected plays, and to show how it functions to create empathy on the part of the reader which helps her/him to internalyse the themes conveyed. Furthermore, this essay intends to stimulate further research on narrative style in Swahili drama.
3

Uhakiki wa tamthilia za kiswahili zihusuzo VVU/UKIMWI

Nicolini, Cristina 10 March 2017 (has links)
Makala haya yanalenga kuchambua fani na maudhui, muundo na dhamira za tamthilia za Kiswahili zihusuzo VVU/UKIMWI, hasa tamthilia kutoka Tanzania, na uhusiano baina ya VVU/UKIMWI na mila za jadi kama sherehe za jando na unyago. Dhamira muhimu ya kujadili ugonjwa katika kazi za fasihi barani Afrika ilichimbuka katika sanaa za maonyesho ya jadi ya Kiafrika yaani katika shughuli za ngoma na miviga ya kidini kama matambiko kwa miungu, kumtolea Mungu kafara ili mgonjwa apate dawa au kupona. Maudhui yanayohusu ugonjwa yameingia katika tamthilia mamboleo kwa nia ya kuoanisha tamthilia ya kigeni na ngoma ya kijadi, hasa baada ya miaka ya 1980 (ling. Mlama 1983; Hussein 1983). Katika tamthilia za Tanzania za kisasa magonjwa yanayozungumziwa ni mengi, lakini kuanzia miaka ya themanini ugonjwa mpya, yaani VVU/UKIMWI, unachukua nafasi ya dhamira kuu katika kazi nyingi. Lengo kuu la makala haya ni kuchambua na kuhakiki tamthilia teule sita zihusuzo VVU/UKIMWI na kuandikwa zote na waandishi wa kutoka Tanzania. Ninachambua vipengele mbalimbali vya fani na maudhui nikiangalia uhusiano baina ya sifa za kimapokeo na za mamboleo. Ninafafanua pia athari za kimagharibi kutoka tamthilia ya Wayunani yaani vigezo vya Aristotle na dhana ya tanzia. Kwa kuunganisha nadharia za kale za Kimagharibi na za kisasa kutoka Afrika Mashariki, nitatumia pia nadharia ya korasi (Mutembei 2012), na vilevile kuchambua athari za ki-Brecht yaani ukengeushi ambazo zimekuwa na umuhimu mkubwa kwa tamthilia ya kutoka nchini kwingi Afrika na ulimwenguni kote.
4

Kumbukizi ya marehemu mwalimu Edwin Semzaba

Godwin Mahenge, Elizabeth, Mbogo, Emmanuel 10 March 2017 (has links) (PDF)
Pumzika kwa amani, Mwalimu. Raha ya milele umpe, Ee Bwana, na mwanga wa milele umwangazie. Amina.
5

Kumbukizi ya marehemu mwalimu Edwin Semzaba

Godwin Mahenge, Elizabeth, Mbogo, Emmanuel 10 March 2017 (has links)
Pumzika kwa amani, Mwalimu. Raha ya milele umpe, Ee Bwana, na mwanga wa milele umwangazie. Amina.

Page generated in 0.0595 seconds