Tamthilia ya Kiswahili imedhihirisha, kwa njia moja au nyingine, uhusiano wa kimwingilianomatini. Makala haya yanadhamiria kuchunguza viwango na aina za mwingilianomatini baina ya tamthilia mbili za Kiswahili. Tamthilia hizi ni Mashetani (Hussein 1971) na Kijiba cha Moyo (Arege 2009). Tathmini hii inaongozwa na nadharia ya mwingilanomatini. Tumeteua na kuhakiki tamthilia hizi kwa misingi kwamba, kwa muda mrefu, Ebrahim Hussein ameaminika kuwa mmojawapo wa watunzi bora wa tamthilia ya Kiswahili katika eneo la Afrika Mashariki. Wahakiki wa fasihi wanaelekea kukubalia na kwamba Ebrahim Hussein ameathiri watunzi wengi wa baadaye wa tamthilia kimtindo, kimaudhui na usawiri wahusika. Lengo la makala haya ni kujaribu kuonesha jinsi tamthilia za Mashetani na Kijiba cha Moyo zinavyofanana kwa kuchunguza viwango vya mwingilianomatini baina ya tamthilia hizo kwa kurejelea, motifu, maudhui, matumizi ya lugha, na wahusika. Je, ni kwa kiwango gani mtunzi wa Kijiba cha Moyo ameathiriwa na mtunzi wa Mashetani? Je, amemnukuu, kudondoa au kumwiga mtangulizi wake kwa kiwango gani?
Identifer | oai:union.ndltd.org:DRESDEN/oai:qucosa.de:bsz:15-qucosa-199683 |
Date | 30 March 2016 |
Creators | Ngesa, Ambrose K., Matundura, Enock, Kobia, John |
Contributors | Moi University,, Universität Leipzig, Institut für Afrikanistik |
Publisher | Universitätsbibliothek Leipzig |
Source Sets | Hochschulschriftenserver (HSSS) der SLUB Dresden |
Language | Swahili (individual language) |
Detected Language | Unknown |
Type | doc-type:article |
Format | application/pdf |
Source | Swahili Forum 22 (2015), S. 42-71 |
Page generated in 0.0026 seconds