Wataalamu mbalimbali wamefafanua dhana ya hadithi fupikwa namna mbalimbali. Kipera hiki cha fasihi andishi ni zao la athari za kimagharibi. Hadithi za fasihi simulizi zimerutubisha hadithi fupi zinazoendeleza majukumu ya tangu jadi ya kuelimisha, kuongoza, kuonya na kuburudisha. Hadithi fupi ya kisasa ina sifa za matumizi ya lugha ya nathari, masimulizi mafupi aghalabu ya tukio moja, mhusika mkuu mmoja au wahusika wachache, msuko sahili na hatimaye mshikamano na umoja wa mawazo na mtindo. Katika makala haya, tunachambua hadithi teule za Kiswahili kuhusu nafasi na ujitambuzi wa wanawake. Kachukua Hatua Nyingine ya Kyallo Wadi Wamitila inajadili hatua ambazo mwanamke anafaa azichukue ili ajikwamue na utumwa wa ndoa zinazompa mwanamume uwezo wote. Nayo Ngome ya Nafsi ya Clara Momanyi inaonyesha hatua anazochukua mtoto msichana kujikomboa dhidi ya mila na desturi zinazomnyima utambulisho wa kibinafsi na kijinsia. Wasia wa Baba ya Ahmad Kipacha inaonyesha jinsi utamaduni na mafundisho chanya ya dini kuwa njia mwafaka za kujengea utambulisho wa mwanamke. Hatimaye Usia wa Mama ya Fatima Salamah inaonyesha mtoto msichana akijihami kupitia utamaduni na mafundisho chanya ya dini dhidi ya ushawishi hasi wa mamake.
Identifer | oai:union.ndltd.org:DRESDEN/oai:qucosa.de:bsz:15-qucosa-137498 |
Date | 27 March 2014 |
Creators | Timammy, Rayya, Swaleh, Amiri |
Contributors | University of Nairobi,, Universität Leipzig, Institut für Afrikanistik |
Publisher | Universitätsbibliothek Leipzig |
Source Sets | Hochschulschriftenserver (HSSS) der SLUB Dresden |
Language | English |
Detected Language | Unknown |
Type | doc-type:article |
Format | application/pdf |
Source | Swahili Forum 20 (2013), S. 102-114 |
Page generated in 0.0219 seconds