Kwanzaa ni sikukuu ya utamaduni pendwa inayosherehekewa na amarekani-Waafrika na watu wengine wa diaspora sehemu mbalimbali duniani. Kwanzaa husherehekewa kwa siku saba toka Desemba tarehe 26 hadi Januari 1. Sherehe hiyo iliyotokana na vuguvugu la Wamarekani weusi kuenzi historia na utamaduni wao toka Afrika. Ilianzishwa mwaka 1966. Katika makala haya, tutaonyesha kwamba Kiswahili katika sherehe hiyo hakitumiki kama lugha ya mawasiliano, kinatumika kama lugha ya kuungana Wamarekani weusi na kuwakumbusha asili zao za kiafrika. Tutaangalia pia maoni mbali mbali ya Waafrika wanaojua Kiswahili na wanaoishi barani Afrika kuhusu sherehe hiyo. Tumeyachukua na tumeyachanganua maoni ya Waghana kwa sababu Ghana ilichaguliwa na watu wa diaspora na hasa na Warasta kama “nchi au ardhi ya rejeo”, kwa hivyo Waghana wanahusika sana na msukumo huu wa Wamarekani weusi.
Identifer | oai:union.ndltd.org:DRESDEN/oai:qucosa.de:bsz:15-qucosa-98364 |
Date | 03 December 2012 |
Creators | Ferrari, Aurelia |
Contributors | University of Ghana, Legon, Department of Modern Languages, Faculty of Arts, Universität Mainz, Insitut für Ethnologie und Afrikastudien |
Publisher | Universitätsbibliothek Leipzig |
Source Sets | Hochschulschriftenserver (HSSS) der SLUB Dresden |
Language | fra |
Detected Language | Unknown |
Type | doc-type:article |
Format | application/pdf |
Source | Swahili Forum; 18(2011), S. 5-23 |
Page generated in 0.0024 seconds