Watumishi wa Taasisi ya Mambo ya Kiafrika ya Chuo Kikuu cha Humboldt walipotayarisha kuhama kwa taasisi yao kutoka
Reinhardtstrasse mwaka 1995, boksi la jivu ilipatikana ndani
ya kabati la chuma. Ndani yake zilihifadhiwa nyaraka za Kiswahili na
Kiarabu zilizoandikwa kwa hati za Kiarabu. Kufuatana na lugha na
maelezo yalioyoongezwa nyaraka hizo zilitoka Afrika Mashariki na
kukusanywa na Gustav Neuhaus mwishoni mwa karne iliyopita. Lengo
la makala hii ni yafuatayo: kutoa maelezo machache juu ya maisha ya
Gustav Neuhaus, kuzungumzia matoleo yake ili kufafanua mchango
wake katika masomo ya Kiswahili mjini Berlin na katika kupanua ujuzi
juu ya lugha na utamaduni wa Waswahili, kutumia mada ya utumwa
kama ilivyoelezwa katika nyaraka mbalimbali za mkusanyo wa Neuhaus
ili kuonyesha umuhimu wa nyaraka hizo kwa historia ya Afrika Mashariki.
Identifer | oai:union.ndltd.org:DRESDEN/oai:qucosa.de:bsz:15-qucosa-94706 |
Date | 23 August 2012 |
Creators | Bromber, Katrin |
Contributors | Zentrum Moderner Orient,, Universität Mainz, Insitut für Ethnologie und Afrikastudien |
Publisher | Universitätsbibliothek Leipzig |
Source Sets | Hochschulschriftenserver (HSSS) der SLUB Dresden |
Language | Swahili (individual language) |
Detected Language | Unknown |
Type | doc-type:article |
Format | application/pdf |
Source | Swahil Forum 6 (1999), S. 175-182 |
Page generated in 0.0019 seconds