361 |
Mgullu, Richard S. 1999. Mtalaa wa isimu: fonetiki, fonolojia na mofolojia ya kiswahili. Nairobi: Longhorn Publishers. Kurasa xv, 247.Ngonyani, Deogratias 30 November 2012 (has links)
Kitabu hiki kinaleta matumaini makubwa ya kuwawezesha wengi ku-soma juu ya lugha yao na kuamsha hamasa ya kujifunza zaidi juu ya lugha hii tukufu na lugha nyingine za kiafrika.
|
362 |
Mara tena juu ya usarufishaji (suala la mwana)Gromova, Nelli V. 30 November 2012 (has links)
Dhana ya usarufishaji, kama Kamusi ya Isimu na Lugha inavyoeleza, ni ubadilishaji wa neno huru ama mofimu huru yenye maana ya kisemantiki na kuifanya mofimu funge na yenye maana ya kisarufi zaidi.
Tunaposema kuhusu usarufishaji, mara nyingi tunamaanisha hasa
ubadilishaji wa neno huru liwe mofimu. Miongoni mwa aina zote za maneno, ambazo zinaweza kusarufishwa, zile zinazotumika mara nyingi zaidi ni nomino na vitenzi. Ningetaka kujibu swali juu ya kazi ya kisarufi ya leksimu mwana: baada ya kuzichunguza maana zake za kisarufi inawezekana kutilia mkazo kwamba katika lugha ya Kiswahili tunashuhudia mwanzo wa kuibadilisha nomino huru mwana iwe kiambishi awali cha uundaji wa maneno mapya yanayotaja watu mbalimbali kutokana na kazi, shughuli zao, kuwepo katika vyama n.k. Inawezekana kwamba maneno ambatani yanayoanzia na mwana
yanaunda ngeli maalum ya nomino (sawa na ngeli ya 1a/2a ya lugha
nyingine za Kibantu).
|
363 |
Tafsiri mpya za fasihi ya Kirusi katika KiswahiliGromova, Nelli V. 30 November 2012 (has links)
Sehemu muhimu ya fasihi andishi ya Kiswahili yachukuliwa na fasihi iliyotafsiriwa kutoka lugha za kigeni. Ingawa vitabu vingi vilikuwa vimetafsiriwa na wageni, Waswahili walio maarufu walishugulika vile vile na kazi hiyo ya kufasiri kama wale Shaaban Robert anayehesabika kuwa mwanzilishi wa fasihi ya kisasa ya Kiswahili pamoja na rais wa kwanza wa Tanzania, baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere. Aidha, vitabu vya fasihi ya Kirusi zilianza kutafsiriwa kuanzia miaka ya sabini karne iliyopita. Nia yangu ilikuwa ni kuvuta uangalifu wa watafsiri Waswahili, kuwasaidia waelewe zaidi matini ya Kirusi na kuizingatia kwa makini katika kuendeleza kazi yao ya ufasiri yenye maana kubwa.
|
364 |
Uzingatifu wa sarufi katika tafsiriKihore, Yared M. 30 November 2012 (has links)
Sarufi inafafanuliwa kama kanuni, sheria au taratibu zinazotawala katika viwango vyote vya uchambuzi wa lugha ambavyo ni umbosauti (au fonolojia), umboneno (au mofolojia), miundomaneno (au sintaksia) na umbomaana (au semantiki). Kuhusiana na masuala ya tafsiri, kanuni muhimu sana zinazopaswa kuzingatiwa ni zile za kiwango cha miundomaneno au sentensi. Kanuni katika kiwango cha miundomaneno, kwa jumla, huwa zinahusu uchaguzi wa maneno sahihi katika muktadha wa maelezo na jinsi maneno kama hayo yanavyopangiliwa kuunda vipashio mbalimbali vya sentensi na sentensi zenyewe. Kwa jumla, huwa kuna aina mbili za tafsiri: tafsiri halisi na tafsiri huru. Nasution 1988 hufikiri kwamba aina hizi mbili za tafsiri hukinzana.
|
365 |
Swahili and the InternetSchmitt, Eleonore 30 November 2012 (has links)
Everybody knows the Intemet by now, most of us have had a glimpse into it or use it frequently. Without doubt it offers many possibilities, like sending long documents within a very short time and without any material carrier from one computer to another or to many others. The World Wide Web (WWW) is an important means of finding information on nearly everything, the web sites are often designed attractively and many offer multi-medial information at the same time. Yet, after a time of euphoria about the possibilities people became aware that the web is very vast and one can spend hours and hours looking for something, without finding it. Roger Pfister with his `Internet for Africanists and others interests in Africa` (see the review in this issue), was a first and most useful attempt to help everybody interested in African studies to find information faster.
|
366 |
Vitendawili vya Kiswahili: usambamba wake na dhima yake katika jamiiNgonyani, Deo 03 December 2012 (has links)
Vitendawili vya Kiswahili, kama vitendawili katika lugha nyingine za Kibantu, na kwa hakika katika lugha nyingine za Kiafrika, ni mafumbo ambayo hutolewa kama kauli au swali linalotaka jibu (Gowlett 1979; Harries 1971, 1976; Okpewho 1992). Vitendawili katika Kiswahili ni sehemu muhimu sana ya michezo ya watoto. Katika jamii ambazo bado zinaishi maisha ya jadi, watoto hukaa pamoja jioni pengine wakiwa na dada zao, kaka zao, na binamu zao wakasimuliana hadithi na kutegana vitendawili. Makala hii inachunguza muundo wa visabiki vya vitendawili vya Kiswahili na kutokana na mchangamano wa muundo tunapendekeza kwamba vitendawili ni njia kuu ya kufundisha watoto ufasaha wa lugha. Ukichunguza usambamba katika vitendawili utaona changamoto kubwa hutolewa kwa mtegaji na wasikilizaji wake kutokana na usambamba ulioko katika sintaksia, fonolojia, kadhalika sitiari. Kama Scheub (2002:124) asemavyo: «Vitendawili ni modeli kwa ajili sanaa za lugha».
|
367 |
Yakobo Lumwe `Eine Reise nach Bukoba`: ReviewKlein-Arendt, Reinhard 03 December 2012 (has links)
Review: Yakobo Lumwe: Eine Reise nach Bukoba, übersetzt und bearbeitet von Ernst Dammann, Wilhelm Fink Verlag,München 1996.
|
368 |
Roger Pfister: Internet for Africanists and Others Interested in Africa.: An Introduction to the Internet and a Comprehensive Compilation of Relevant Addresses. A Review.Schmitt, Eleonore 03 December 2012 (has links)
Scientists make use of the Internet for quite some time now. In the humanities it has only recently become accepted more widely. The Swiss Society of African Studies reacted sceptically when Roger Pfister first introduced his project. In. his preface, Beat Sottas, the society`s president admits that their committee was `wondering about such a project`but that finally the `initiative turned out to be highly significant at the time being.
|
369 |
Swahilité in the French Comorian DiasporaEnglert, Birgit 05 June 2023 (has links)
In her article, Daniela Waldburger argued for the inclusion of varieties from the Greater Swahili Area in Swahili lessons. She discussed what it means to be a Mswahili and argued that while identification as a Mswahili can be linked to various aspects, competence in Swahili remains unquestioned as a necessary condition for identification as a Mswahili. In this paper, I would like to go a step further and question the relationship between competence in the Swahili language and the relevance of the notion of Swahili nature or Swahilité to a person. More specifically, I would like to reflect on the relevance of the notion of Swahilité in a diasporic space, more precisely the Franco-Comorian community in France, drawing on data from fieldwork in Bordeaux (2010 and 2011) and Marseille (2012).
|
370 |
Syntactic and semantic underspecification in the verb phraseMarten, Lutz January 1999 (has links)
No description available.
|
Page generated in 0.0536 seconds