• Refine Query
  • Source
  • Publication year
  • to
  • Language
  • 473
  • 161
  • 70
  • 70
  • 24
  • 18
  • 11
  • 8
  • 1
  • 1
  • 1
  • 1
  • 1
  • 1
  • 1
  • Tagged with
  • 699
  • 612
  • 602
  • 328
  • 327
  • 327
  • 169
  • 152
  • 148
  • 88
  • 76
  • 71
  • 71
  • 68
  • 67
  • About
  • The Global ETD Search service is a free service for researchers to find electronic theses and dissertations. This service is provided by the Networked Digital Library of Theses and Dissertations.
    Our metadata is collected from universities around the world. If you manage a university/consortium/country archive and want to be added, details can be found on the NDLTD website.
191

Kiswahili Research in Kenyan Universities:

Ngugi, P.M.Y., Masau, P.M. 30 November 2012 (has links) (PDF)
The Department of Linguistics and African Languages, in which Kiswahili is a central subject, was established in the Faculty of Arts at the University College of Nairobi in 1969. Since then, at least five more departments which are devoted to the teaching and study of the Kiswahili language and literature have been established in various Kenyan universities (see below). Most of these departments run post-graduate programmes leading to MA. and PhD - degrees. As a result, considerable research activity related to both the Kiswahili language and literature has been going on. This is evident from the dissertations that have been written and that continue to be written every year.
192

Hali ya vitabu vya watoto katika Tanzania

Madmulla, J. S. 30 November 2012 (has links) (PDF)
Makala haya yamekusudia kujadili hali ya vitabu vya watoto katika Tanzania. Lengo letu ni kutathmini, kwa namna fulani, hali ya ujenzi wa elimu ya msingi katika nchi yetu, matatizo yanayokwamisha kustawi kwa elimu ya msingi na namna ya kuyapatia suluhu. Katika juhudi za kutafuta suluhu, tutaeleza namna Mradi wa Vitabu vya watoto unavyotoa mchango wake mkubwa. Hata hivyo, itafaa tuanze kwa kupitia historia fupi ya vitabu vya watoto katika Tanzania.
193

Mgullu, Richard S. 1999. Mtalaa wa isimu: fonetiki, fonolojia na mofolojia ya kiswahili. Nairobi: Longhorn Publishers. Kurasa xv, 247.

Ngonyani, Deogratias 30 November 2012 (has links) (PDF)
Kitabu hiki kinaleta matumaini makubwa ya kuwawezesha wengi ku-soma juu ya lugha yao na kuamsha hamasa ya kujifunza zaidi juu ya lugha hii tukufu na lugha nyingine za kiafrika.
194

Mara tena juu ya usarufishaji (suala la mwana)

Gromova, Nelli V. 30 November 2012 (has links) (PDF)
Dhana ya usarufishaji, kama Kamusi ya Isimu na Lugha inavyoeleza, ni ubadilishaji wa neno huru ama mofimu huru yenye maana ya kisemantiki na kuifanya mofimu funge na yenye maana ya kisarufi zaidi. Tunaposema kuhusu usarufishaji, mara nyingi tunamaanisha hasa ubadilishaji wa neno huru liwe mofimu. Miongoni mwa aina zote za maneno, ambazo zinaweza kusarufishwa, zile zinazotumika mara nyingi zaidi ni nomino na vitenzi. Ningetaka kujibu swali juu ya kazi ya kisarufi ya leksimu mwana: baada ya kuzichunguza maana zake za kisarufi inawezekana kutilia mkazo kwamba katika lugha ya Kiswahili tunashuhudia mwanzo wa kuibadilisha nomino huru mwana iwe kiambishi awali cha uundaji wa maneno mapya yanayotaja watu mbalimbali kutokana na kazi, shughuli zao, kuwepo katika vyama n.k. Inawezekana kwamba maneno ambatani yanayoanzia na mwana yanaunda ngeli maalum ya nomino (sawa na ngeli ya 1a/2a ya lugha nyingine za Kibantu).
195

Tafsiri mpya za fasihi ya Kirusi katika Kiswahili

Gromova, Nelli V. 30 November 2012 (has links) (PDF)
Sehemu muhimu ya fasihi andishi ya Kiswahili yachukuliwa na fasihi iliyotafsiriwa kutoka lugha za kigeni. Ingawa vitabu vingi vilikuwa vimetafsiriwa na wageni, Waswahili walio maarufu walishugulika vile vile na kazi hiyo ya kufasiri kama wale Shaaban Robert anayehesabika kuwa mwanzilishi wa fasihi ya kisasa ya Kiswahili pamoja na rais wa kwanza wa Tanzania, baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere. Aidha, vitabu vya fasihi ya Kirusi zilianza kutafsiriwa kuanzia miaka ya sabini karne iliyopita. Nia yangu ilikuwa ni kuvuta uangalifu wa watafsiri Waswahili, kuwasaidia waelewe zaidi matini ya Kirusi na kuizingatia kwa makini katika kuendeleza kazi yao ya ufasiri yenye maana kubwa.
196

Chachage Seithy L. Chachage: Makuadi wa soko huria (2002). Uchambuzi na uhakiki.

Mbonde, John P. 30 November 2012 (has links) (PDF)
Chachage Seithy L. Chachage amepata kuandika riwaya nyingine tatu: Sudi ya Yohana (1980), Kivuli (1984) na Almasi za Bandia (1990). Riwaya yake ya nne Makuadi wa Soko Huria (2002) ni ya kihistoria na yenye upekee wa maudhui, muundo na mtindo. Vipengele hivi vinadhihirisha ukomavu na upeo wa juu wa mwandishi ilimradi kwenda sambamba na changamoto ya utandawazi ya karne ya ishirini na moja ya milenia ya tatu. Mwandishi amekitabaruku kitabu hiki kwa kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (1922-1999).
197

Uzingatifu wa sarufi katika tafsiri

Kihore, Yared M. 30 November 2012 (has links) (PDF)
Sarufi inafafanuliwa kama kanuni, sheria au taratibu zinazotawala katika viwango vyote vya uchambuzi wa lugha ambavyo ni umbosauti (au fonolojia), umboneno (au mofolojia), miundomaneno (au sintaksia) na umbomaana (au semantiki). Kuhusiana na masuala ya tafsiri, kanuni muhimu sana zinazopaswa kuzingatiwa ni zile za kiwango cha miundomaneno au sentensi. Kanuni katika kiwango cha miundomaneno, kwa jumla, huwa zinahusu uchaguzi wa maneno sahihi katika muktadha wa maelezo na jinsi maneno kama hayo yanavyopangiliwa kuunda vipashio mbalimbali vya sentensi na sentensi zenyewe. Kwa jumla, huwa kuna aina mbili za tafsiri: tafsiri halisi na tafsiri huru. Nasution 1988 hufikiri kwamba aina hizi mbili za tafsiri hukinzana.
198

Vitendawili vya Kiswahili: usambamba wake na dhima yake katika jamii

Ngonyani, Deo 03 December 2012 (has links) (PDF)
Vitendawili vya Kiswahili, kama vitendawili katika lugha nyingine za Kibantu, na kwa hakika katika lugha nyingine za Kiafrika, ni mafumbo ambayo hutolewa kama kauli au swali linalotaka jibu (Gowlett 1979; Harries 1971, 1976; Okpewho 1992). Vitendawili katika Kiswahili ni sehemu muhimu sana ya michezo ya watoto. Katika jamii ambazo bado zinaishi maisha ya jadi, watoto hukaa pamoja jioni pengine wakiwa na dada zao, kaka zao, na binamu zao wakasimuliana hadithi na kutegana vitendawili. Makala hii inachunguza muundo wa visabiki vya vitendawili vya Kiswahili na kutokana na mchangamano wa muundo tunapendekeza kwamba vitendawili ni njia kuu ya kufundisha watoto ufasaha wa lugha. Ukichunguza usambamba katika vitendawili utaona changamoto kubwa hutolewa kwa mtegaji na wasikilizaji wake kutokana na usambamba ulioko katika sintaksia, fonolojia, kadhalika sitiari. Kama Scheub (2002:124) asemavyo: «Vitendawili ni modeli kwa ajili sanaa za lugha».
199

Mabadiliko katika umbo la ushairi na athari zake katika ushairi wa Kiswahili

Indede, Florence Ngesa 03 December 2012 (has links) (PDF)
Mwanadamu amejaribu kwa vyovyote vile kuvumbua na kunyumbua mambo mapya ambayo yataleta mvuto na kupimia akili yake kiubunifu katika hali ya kutaka kutangamana zaidi na binadamu mwenzake au kutaka kuelewa zaidi ulimwengu wake. Ndiposa washairi wengi wa kisasa wanashikilia kwamba ulimwengu unabadilika na hivyo utamaduni wa ushairi lazima ubadilike. Katika wasilisho hili tunajadili mabadiliko haya ya kimaumbo na athari zake katika ushairi wa Kiswahili. Si lengo letu kushawishi msomaji kujiunga na kikundi fulani cha ushairi bali kuangazia hoja mwafaka zinazotokana na mivutano na mikinzano katika mabadiliko haya, na namna mitazamo hii inavyofanikisha maendeleo ya ushairi.
200

In Memorian Andrej Aleksejevic Zhukov

Miehe, Gudrun 14 December 2012 (has links) (PDF)
Obituary for Andrej Aleksejevic Zhukov

Page generated in 0.0334 seconds