• Refine Query
  • Source
  • Publication year
  • to
  • Language
  • 100
  • 20
  • 16
  • 8
  • 8
  • 3
  • 2
  • 1
  • 1
  • Tagged with
  • 143
  • 71
  • 65
  • 50
  • 48
  • 33
  • 33
  • 33
  • 18
  • 18
  • 17
  • 14
  • 9
  • 8
  • 8
  • About
  • The Global ETD Search service is a free service for researchers to find electronic theses and dissertations. This service is provided by the Networked Digital Library of Theses and Dissertations.
    Our metadata is collected from universities around the world. If you manage a university/consortium/country archive and want to be added, details can be found on the NDLTD website.
71

Nafasi ya muziki uliopendwa katika fasihi ya kiswahili

Ngugi, Pamela M. Y. 30 November 2012 (has links) (PDF)
Nyimbo, kama tanzu ya fasihi yeyote ile zina majukumu mbalimbali ambayo hutekeleza katika jamii. Lengo kuu la fasihi ni lile la kuielimisha na hata kuiburudisha jamii. Ndivyo ilivyo katika nyimbo kwa sababu kupitia kwazo wanajamii huburudika na kuelimishwa. Ni kwa sababu hiyo ndipo makala hii inalenga kuangalia nafasi ya nyimbo zinazopendwa katika fasihi ya Kiswahili. Huu ni utanzu ambao huwafikia watu wengi katika jamii. Kutokana na kutumia lugha ya Kiswahili, utanzu huu unaweza kueleweka na Wakenya wengi. Nchini Kenya, vyombo vya habari vimeipa fasihi hii nafasi kubwa sana na hivyo basi kuipanua hadhira yake. Hii ni kutokana na sababu kuwa fasihi hii inathaminiwa sana na wengi na ipewe nafasi kubwa katika vyombo vya habari hasa katika redio kwa muda mrefu. Ni kutokana na sababu hii ndipo tunajaribu kuonyesha nafasi yake katika fasihi ya Kiswahili.
72

Utegemezi au utegemeano baina ya Kenya na Tanzania katika ukuzaji na uendelezaji wa Kiswahili nchini Kenya?

Oyori Ogechi, Nathan 14 December 2012 (has links) (PDF)
Makala haya yanatathmini iwapo ukuzaji na uendelezaji wa Kiswahili nchini Kenya unategemea shughuli za kuiendeleza lugha hii zinazofanywa na Tanzania ama unatokana na kutegemeana baina ya mataifa haya katika kukikuza na kukiendeleza Kiswahili. Baadhi ya njia za kuiendeleza lugha zinajumuisha: kuisanifisha, kuifanyia utafiti na kuiimarisha kwa kuitungia kamusi, vitabu vya sarufi, kazi za kisanaa na kuitumia serikalini, mahakamani, katika elimu n.k. Makala haya yanaonyesha kuwa ingawa kuna utegemeano kati ya Kenya na Tanzania katika ukuzaji na uendelezaji wa Kiswahili, Tanzania inategemewa zaidi. Hususan inadhahirishwa kuwa Kenya imeitegemea Tanzania kwa kuagizia machapisho, wataalamu wa Kiswahili mbali na kutumia istilahi na hata kuchuma nafuu mifano ya Tanzania katika utumishi wa umma. Fauka ya hayo, inaonyeshwa kuwa pale ambapo Kenya haijafaidi kutokana na ufanisi wa Tanzania, ikiiga mfano wa Tanzania, upo uwezekano wa kufaulu.
73

Memory in translation: Mau Mau Detainee and its Swahili Translation

Aiello Traoré, Flavia 31 March 2015 (has links) (PDF)
Enzi baada ya uhuru baadhi ya tafsiri mpya kwa Kiswahili zilianza kutokea nchini Kenya, zikiwemo tafsiri za riwaya na tawasifu za waandishi Wakenya. Makala haya yanazingatia tawasifu ya Josiah Mwangi Kariuki iitwayo Mau Mau Detainee (1963) inayosimulia kumbukumbu za mateso aliyoya-pata mwandishi mwenyewe wakati wa miaka ya hali ya hatari, na tafsiri yake kwa Kiswahili yaani Mau Mau Kizuizini (1965) iliyofasiriwa na Joel Maina. Kwanza, tawasifu ya Mau Mau Detainee itachambuliwa kwa kujikita hasa katika jinsi mwandishi mwenyewe alivyobuni lugha changamano takitumia Kiingereza kinachochanganywa na Kigĩkũyũ pamoja na Kiswahili. Halafu, tafsiri yake ii-wayo Mau Mau Kizuizini itachambuliwa kwa kina kwa ajili ya kuanza kufafanua jinsi na kwa mbinu gani mfasiri alivyokabiliana na vipengele vya pekee vya matini hiyo wakati alipokuwa anatafsiri kumbukumbu hizo za ukoloni akiwa anawalenga wasomaji wa lugha pokezi.
74

Swahili popular literature in recent years

Gromov, Mikhail D. January 2008 (has links)
The article outlines recent trends in popular writing in Swahili in Kenya and Tanzania, the research being mainly based on titles published after the year 2000, by both well-known writers and newcomers. The author also generalises on some basic social and cultural factors accountable for the present state of popular literature in both countries.
75

What's wrong with the Marine and the beauty?

Bertoncini-Zúbková, Elena 15 August 2012 (has links) (PDF)
Instead of discussing an outstanding literary work by a well-known Swahili writer, this time I would like to present a second- or third-rate book by a renownless author (at least to my knowledge), Gilbert Gicaru Githere.2 Its title is Mwana Maji na Mrembo (The Marine and the beauty). It was published in 1990 by an otherwise unknown publishing house, Merengo Publishers, and printed in Hawaii. I have chosen this book because, in spite of its many flaws, it has some interesting features: The whole novel is written almost as a film script; descriptions of actions and landscapes are film-like, and the characters are seen as if they were on the screen. The problem is that this narrative technique does not work, so I want to analyse what is wrong with it.
76

Publishing in Kiswahili and indigenous languages for enhanced adult literacy in Kenya

Ogechi, Nathan Oyori 09 August 2012 (has links) (PDF)
This paper argues a case for the preparation of reading materials in Kiswahili and other African languages in order to enhance adult education in Kenya. Adult education clientele are defined as those aged over 15 who (a) were either never enrolled in primary schools or dropped out before completing and (b) `graduated` and currently participate in community extension services. Cognisance of mothertongues as the best languages to begin basic literacy is taken. However, since the literacy so acquired should be useful to the individual at both local and national levels, one needs Kiswahili for wider communication. Therefore, reading materials, especially for post literacy and adult literacy teacher training should be in Kiswahili. This will not only guard against relapsing to illiteracy and misinformation but will also alleviate the scarcity of reading materials in the face of hard economic times in Kenya.
77

Mahojano na Ben R. Mtobwa

Gromov, Mikhail D. 03 December 2012 (has links) (PDF)
Mahojiano haya yamefanyika tarehe 11 Januari 2008, mjini Mainz, Ujerumani, wakati wa Kongamano la Tisa la Janheinz Jahn “Beyond ‘murder by magic’: investigating African crime fiction” lililofanyika Chuo Kikuu cha Mainz.
78

Ujuzi wa watoto/vijana katika simulizi za maisha

Schulz-Burgdorf, Ulrich 14 December 2012 (has links) (PDF)
Kutoka elimu ya lugha tunajua kwamba kila mtu aliyenena ana ujuzi maalum - kama John Lyons alivyoeleza katika kitabu chake Language and Linguistics (1981), katika sura kuhusu lugha na utamaduni wa wasemaji. Lyons anatueleza kwamba kila mtu hushika ujuzi huo kwa njia ya kufunzwa lugha na huutumia ujuzi, huuongeza na huubadilisha kwa muda wa maisha yake yote; ni jinsi yake ya kujua mambo ya ulimwengu. Katika maelezo yafuatayo napenda kuonyesha ujuzi uliomo katika habari nilizopewa na kijana, jina lake ni Timothy Lawrence ambaye alikuwa na umri wa kumi na tatu siku zile. Ujuzi wake ni juu ya maisha yake ya kipokomo na pia ni ujuzi wa kumweleza mgeni mambo hayo - yaani ujuzi au uwezo wa kuzisimulia habari hizo. Habari zake zinatuonyesha vizuri simulizi ya maisha ya binafsi (au autobiographical narrative) ni nini, yenye ujuzi gani na jinsi gani ya kutazama maisha kwa macho ya mwenyeji kijana.
79

Kutoka lugha kienzo hadi lugha ya isimu: matatizo yanayotinga kiswahili kama lugha ya kufunzia isimu vyuoni vikuu nchini Kenya

Mbatha Mathooko, Petronilla 14 December 2012 (has links) (PDF)
Makala hii inachunguza hali ya somo la isimu ya lugha linalofundishwa katika nyingi ya idara za Kiswahili vyuoni vikuu nchini Kenya. Inaangazia matatizo yanayotinga kufana kwa somo hili. Inahitimiza kwa kupendekeza kwamba iwapo matokeo mazuri yatapatikana na wanafunzi wa somo hili, yafaa matatizo yanayokwamiza somo hili yatatuliwe, hasa kwa upande wa usawazishaji wa istilahi, tafsiri, uzito wa kozi na mengineyo. Makala hii inapendekeza kuwa ni muhimu kila chuo kikuu kiunde kamati ya kuchunguza jambo hili.
80

Facing the language border: multi-lingualism in two novels of M. G. Vassanji review

Gromov, Mikhail D. 31 March 2015 (has links) (PDF)
The study focuses on the use of various languages including Swahili by the author Moyez G. Vassanji against the English background of his works, by concentrating on two of his ´African´ novels, namely The Gunny Sack and The In-Between World of Vikram Lall. In his novels, Vassanji uses multiple literary devices involving the use of different languages, such as code switching and code shifting among others. The paper analyses the use of these various ´language-mixing´ devices in his novels from a literary point of view. A set of literary instruments allow the author to attain various tasks, such as creating ´local colour´, restoring social relationships, and also expressing the characters´ search for new identity, as well as reflecting the author´s own background as a multi-cultural person and writer.

Page generated in 0.0279 seconds