291 |
Habari za miti na mitishamba miongoni mwa Wamijikenda na Waswahili-matokeo ya kwanza kutoka utafitiSchulz-Burgdorf, Ulrich 30 November 2012 (has links) (PDF)
Utafiti ambao ni msingi wa habari hizo umefanywa katika miezi za Oktoba mpaka Disemba 2000 katika wilaya wa Kwale na Kilifi huko nchi ya Kenya. Wanachama wa timu ya utafiti wetu walikuwa Prof. F. Rottland, ambaye aliweka taratibu msamiati wa miti uliokusanywa, na Bw. Mohamed Pakia ambaye ni mwanabiolojia na aliyehojiana wanafunzi wa shule ya sekondari kuhusu ujuzi wa miti na mitishamba wao. Bw. Pakia ameshafanya kazi katika Coastal Forest Conservation Unit, yaani watu ambao husaidia wazee wa kimijikenda katika kuhifadhi misitu mitakatifu inayoitwa \"makaya\" na inatumiwa kwa matambiko na kama makaburi. Bw. Pakia ametambua: Ni hatari ya kupoteza ujuzi wa miti na mitishamba iliyotumiwa nanma ya kimila miongoni mwa wanafunzi wa shule ya sekondari: vijana hawajui matumizi ya mimea na pia wamepotea moyo wa kutaka kujua mambo hayo. Katika habari zifuatazo ninatoa mifano ya ule ujuzi wa watu wazima na wazee.
|
292 |
Masuala ya kisarufi katika magazeti ya mitaani ya kiswahili - TanzaniaKihore, Yared M. 30 November 2012 (has links) (PDF)
Baada ya kupitishwa kwa sheria iliyoruhusu kuanzishwa kwa magazeti binafsi mnamo 1992, kumeibuka magazeti mengi ya lugha ya Kiswahili nchini Tanzania yanayochapishwa kila siku. Kundi moja la magazeti ni lile la magazeti yanayojulikana kwa jumla kama `Magazeti ya Mitaani´. Magazeti katika kundi hili yanabeba mada nyingi mbalimbali zinazohusu mambo ya watu mitaani, masuala ya mambo ya kidini mitaani, vichekesho, na mara nyingi yale yanayowasibu wanajamii mitaani mmojammoja au kwa jumla. Nia yetu katika makala haya ni kuchunguza masuala ya kisarufi katika maelezo yanayojitokeza katika `magazeti ya mitaani´.
|
293 |
Gabriel Ruhumbika: Janga sugu la wazawa (2002). Uchambuzi na UhakikiMbonde, John P. 30 November 2012 (has links) (PDF)
Gabriel Ruhumbika aliyezaliwa mwaka 1938 kisiwani Ukerewe ni miongoni mwa wanafasihi waliokubuhu katika fani ya riwaya za Kiswahili. Sasa ametuletea riwaya hii ya aina yake Janga sugu la wazawa (2002). Kwa jumla, riwaya hii linaakisi hali halisi ya mfumo wa maisha ya Wakerewe kwa kuwalinganisha na jamii inayokizunguka kisiwa cha Ukerewe, mintarafu imani za jadi na jinsi Ukristo ulivyoathiri misingi hiyo. Hali kadhalika, riwaya hii linasisitiza umuhimu wa kuzingatia kuthamini tamaduni, mila na desturi na maadili mema katika jamii.
|
294 |
L’onomastique comorienne: etude linguistiqueYahaya, Moinaecha Cheikh 03 December 2012 (has links) (PDF)
Dans cette etude nous nous sommes fixé commee objectif principal la recherche des morphèmes nominaux altérés dans la langue courante et qui se manifestent au niveau des noms propres surtout au niveau des composés. Ces éléments nous permettront de mieux comprendre le système morphologique du comorien et compléter une etude en cours sur la morphologie des nominaux. L’étude morphologique du nom propre sera complétée par une étude syntaxique des différents éléments qui le composent. Les indications socio-culturelles et socio-linguistiques étant très significatives, nous introduirons une approche thématique qui nous éclairera un peu sur ce sujet.
|
295 |
Mwili, nafsi na roho katika ugonjwa: mfano wa simulizi za ugonjwa (illness narratives)Schulz-Burgdorf, Ulrich 03 December 2012 (has links) (PDF)
Simulizi za ugonjwa zinatolewa na mgonjwa na mtu mmoja au wengi wanaoombwa naye wamsaidie wakashauriana hali ya maradhi. Kutambua ugonjwa ni kazi ya kawaida na siyo ya waganga au madaktari tu. Kama pengine, katika Afrika ya Mashariki wenyeji huwa na ujuzi wa kawaida juu ya maradhi, mwili, tiba, dawa za hospitali na za kienyeji. Kila jinsi ya tiba ina njia, lugha na mazoezi yake. Mfano ufuatao unaonyesha maana na matumizi ya dhana na tashbihi (metaphors) katika uganga wa kienyeji. Ni kazi yangu sasa ya kufasiri matumizi ya tashbihi na alama katika mawasiliano ambayo huitwa `simulizi za ugonjwa´, yaani illness narratives ambazo ni dhana ya utafiti katika mawasiliano ya kuganga.
|
296 |
Utegemezi au utegemeano baina ya Kenya na Tanzania katika ukuzaji na uendelezaji wa Kiswahili nchini Kenya?Oyori Ogechi, Nathan 14 December 2012 (has links) (PDF)
Makala haya yanatathmini iwapo ukuzaji na uendelezaji wa Kiswahili nchini Kenya unategemea shughuli za kuiendeleza lugha hii zinazofanywa na Tanzania ama unatokana na kutegemeana baina ya mataifa haya katika kukikuza na kukiendeleza Kiswahili. Baadhi ya njia za kuiendeleza lugha zinajumuisha: kuisanifisha, kuifanyia utafiti na kuiimarisha kwa kuitungia kamusi, vitabu vya sarufi, kazi za kisanaa na kuitumia serikalini, mahakamani, katika elimu n.k. Makala haya yanaonyesha kuwa ingawa kuna utegemeano kati ya Kenya na Tanzania katika ukuzaji na uendelezaji wa Kiswahili, Tanzania inategemewa zaidi. Hususan inadhahirishwa kuwa Kenya imeitegemea Tanzania kwa kuagizia machapisho, wataalamu wa Kiswahili mbali na kutumia istilahi na hata kuchuma nafuu mifano ya Tanzania katika utumishi wa umma. Fauka ya hayo, inaonyeshwa kuwa pale ambapo Kenya haijafaidi kutokana na ufanisi wa Tanzania, ikiiga mfano wa Tanzania, upo uwezekano wa kufaulu.
|
297 |
Janzanda ya njozi katika baadhi ya mashairi ya Euphrase Kezilahabi / Oneiric images in Euphrase Kezilahabi´s selected poemsAcquaviva, Graziella 29 August 2012 (has links) (PDF)
This article is based upon the following concept: Poetry is a chain of representation of the sub-conscience that is the creative source. We can read the poetic text in many ways, but if we imagine the text as the stage of images, we can understand the fundamental abstraction of the conscience. In this sense, oneiric images in some of Euphrase Kezilahabi’s poems will be analysed by using insights from psychoanalytic theory.
|
298 |
Memory in translation: Mau Mau Detainee and its Swahili TranslationAiello Traoré, Flavia 31 March 2015 (has links) (PDF)
Enzi baada ya uhuru baadhi ya tafsiri mpya kwa Kiswahili zilianza kutokea nchini Kenya, zikiwemo tafsiri za riwaya na tawasifu za waandishi Wakenya. Makala haya yanazingatia tawasifu ya Josiah Mwangi Kariuki iitwayo Mau Mau Detainee (1963) inayosimulia kumbukumbu za mateso aliyoya-pata mwandishi mwenyewe wakati wa miaka ya hali ya hatari, na tafsiri yake kwa Kiswahili yaani Mau Mau Kizuizini (1965) iliyofasiriwa na Joel Maina. Kwanza, tawasifu ya Mau Mau Detainee itachambuliwa kwa kujikita hasa katika jinsi mwandishi mwenyewe alivyobuni lugha changamano takitumia Kiingereza kinachochanganywa na Kigĩkũyũ pamoja na Kiswahili. Halafu, tafsiri yake ii-wayo Mau Mau Kizuizini itachambuliwa kwa kina kwa ajili ya kuanza kufafanua jinsi na kwa mbinu gani mfasiri alivyokabiliana na vipengele vya pekee vya matini hiyo wakati alipokuwa anatafsiri kumbukumbu hizo za ukoloni akiwa anawalenga wasomaji wa lugha pokezi.
|
299 |
Misemo katika lugha za magari: divai mpya?Kipacha, Ahmad 31 March 2015 (has links) (PDF)
Tangu kuzuka kwa umiliki wa vyombo vya moto vya usafiri (mabasi, malori, pikipiki) kwa watu binafsi katika miaka ya 1990 nchini Tanzania, misemo kwa kiasi kikubwa imechupa kutoka katika majukwaa yake ya asili ya kanga, vihangaisho, vipepeo na makawa majumbani na kuhamia katika vyombo vya usafiri. Si tu misemo mipya imezuka bali hata ile misemo ya asili imepindwa na kutumiwa katika miktadha mipya. Waandishi wa semi za magari ni madereva, utingo au wamiliki wa vyombo hivyo. Tumebaini makundi matatu ya misemo katika data yetu, yaani misemo kongwe, misemo pindwa na misemo ibuka, kwa kuakisi nadharia za methali na misemo za Mieder & Litovkina (1999), Mieder (2007) na Litovkina (2011). Je, misemo hiyo ni mkondo wa fikra mpya za watu kama alivyotabiri Kezilahabi (1988, 1995)? / Since the introduction of the private commercial motor transport services in Tanzania in the 1990s, the inscription of sayings has shifted from their mainly traditional platforms of female cotton wrap (Kanga), palm leaf food cover (kawa) or hand fan (kipepeo) onto the tailgate, sideboards or mudguards of commercial automobiles. The vehicle owners and/or their operators are inscribers of these automobile slogans. I analyse them in three forms: standard, parodied and innovated sayings adopting the paremiological approaches by Mieder & Litovkina (1999), Mieder (2007), Litovkina (2011). Do these forms of car inscriptions fulfill the prediction by Kezilahabi (1988, 1995) on the imminent transformation of the Swahili sayings to become a platform for negotiation of people`s tumultuous life challenges and desires?
|
300 |
On the copula in the Kikae dialect of SwahiliFurumoto, Makoto January 2015 (has links)
The Kikae dialect is a regional variety of Swahili spoken in the southern part of Unguja, the largest island of the Zanzibar archipelago. In this dialect, the morpheme -wa preceded by a subject prefix, which agrees with the subject in person or noun class, is used as a copula. This form is used in neither Standard Swahili nor the Kiunguja dialect considered prestigious dialects of Swahili. In this paper, I describe the morphological and semantic characteristics of this copula, which have not been observed in previous studies, and propose a possible grammaticalisation path of the copula based on its synchronic properties and typological evidence. The following three claims will be made: 1. the subject prefix -wa morphologically corresponds to the perfect form, but does not encode a prior event unlike the perfect form of other verbs. 2. The use of the subject prefix -wa copula is restricted to ‘predicational sentences’. 3. It is highly probable that the subject prefix -wa has grammaticalized from a locative verb
|
Page generated in 0.0343 seconds